Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2021

COP26 Glasgow,Scotland

Picha
         Viongozi na wajumbe kutoka takriban nchi 200 wanakongamana kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya hali ya anga,ambalo limengoa nanga huko Glasgow,Scotland,leo Katika mkutano huu wa COP26, maswala kadha yatajadhiriwa hususan jinsi ya kupunguza utoaji gesi ya carbon kufikia mwaka 2030 na kunusuru dunia kutoa kwa adhari za mabadiliko ya hali ya anga. K ongamano hili litafanyika kwa majuma mawili,huku fursa ya kwanza ikitolewa kwa Shirika la utabiri wa hali ya anga duniani ili kutoa ripoti kuhusu hali ya anga ilivyo kufikia sasa.Lengo likiwa kutathmini viwango vya joto duniani kufikia mwaka huu na miaka ya awali. Zaidi ya hayo, ripoti imeandaliwa na itatolewa na wanasayansi wa hali ya anga. Hali ya anga imebadilika kwa kasi huku shughuli za wanadamu zikitolewa kama chanzo kuu cha mabadiliko hayo. Viwango vya juu zaidi vya joto, mafuriko na moto misituni inazidi kuongezeka,jambo ambalo linatia hofu. Mkutano huu una...

Reuben Githinji

Picha
  Reuben Githinji Ugonjwa wa COVID-19 umetupokonya mwanadishi aliyebombea Reuben Githinji. Githinji aliugua na alihitaji dharula lakini hospitali ya mkoa ya Embu,haikuwa na nafasi. Ilibidi ahamishe hadi Hospitali ya Muranga ambapo alifariki akipokea matibabu. Nimehuzunishwa na kifo cha mtu niliye mfahamu kwa muda mrefu na nilimuita kakangu. Nilikutana naye Reuben Githinhji alipokuwa anandkikia kampuni ya Kenya Times huko Meru. Nilikuwa mwandishi wa Habari aliyekuwa anajifunza uanahabari,hivyo basi baadaya ya rikizo kutoka chuoni tulitakiwa kutafuta nafasi ya miazi nne ili kufijunza nje ya darasa. Kwa bahati nzuri, nilipata nafasi kutoka kwa kampuni ya nation wakanituma, wilaya ya Meru alipokuwa mwanahabari wao Imanene Imathiu ambaye ni marehemu. Katika harakati za kukusanya Habari hapa ana pale nilikutana na Githinji ambaye alikuwa anapenda sana kazi yake. Alipenda sana kuandika kuhusu maswala ya siasa na jamii kwa jumla. Nkumbuka wakati ule Kampuni ya Kenya Tim...

Chebet Karago

Picha
Lala salama Chebet Tangu utotoni,ilikuwa ni ndoto yangu kuwa mwanahabari mashuhuri. Hakika nilipenda sana kuwa mwanahabari. Ndoto yangu ilitimia nilipopata fursa ya kujiunga na Chuo cha Mawasilisano na Utangazaji, K.I.M.C, maeneo ya South C. katika halakati ya masomo,tulitakiwa kutafuta moja wapo ya mashirika au kampuni zinazo chapisha na pia kutangaza habari na matukio tofauti nchi na duniani kwa ujumla. Baada ya kufikiria kwa muda,niliamua kwenda katika kituo cha habari cha Nation. Hapo ndipo nilikutana na wanahabari waliobobea kama vile Caleb Atemi, Marehemu Bob Okoth,Amos Ngaira,Njeri Rugene baadhi wa wanahabari wengine. Aliyenipokuwa hasa kwa mikono miwili alikuwa ni mwendazake Chebet Karago ambaye alinielekeza jinsi ya kuwa mwanahari na kunisaidi sana katika nyaja ya uwanahabari. Mkutano na Chebet. Nilikutana na mwandishi Chebet Karago katika jumba la Nation, nilipokuwa nimeenda kuomba nafasi ya kuandika katika gazeti la Sunday Nation hasa kwenye ukurasa wa Young ...