Jumanne, 29 Novemba 2011

kongamano la uzazi mpango Dakar,Senegal





Kongamano kuhusu afya ya uzazi yaanza leo jijini Dakar nchini Senegal.
Mkutano huu unafanyika huku karibu watu millioni 900 kote duniani wakikumbatia uzazi wa mpango.

Hata hivyo, sio wote wanaoweza kufanya uzazi wa mpango wakati wanapotaka kufuatia changamoto kadha wa kadha.

Mkutano huu utawajumuisha watafiti wa afya,madaktari na wadau wengine katika sekta ya afya.
Kufanyika kwa mkutano huu katika Afrika Magharibi,ni jambo la muhimu ikifahamika kuwa nchi za Afrika Magharibi zinaongoza kwa idadi ya watu kwani mpango wa uzazi ungali haujapewa kipao mbele.
Pia kupata hutuma ya uzazi wa mpango ni shinda.

Inaaminika kuwa wazazi wengi ambao wangependa kupanga uzazi wanasubuka sana.Hata kabla wapate huduma hiyo muhimu wanagundua kuwa ni wajawazito.Idadi ya wanandoa walio kwenye hali hii ni zaidi ya millioni 215 kote duniani.

 Uzazi wa mpango unawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya  ya familia.


Ijumaa, 25 Novemba 2011

FGM (ukeketaji) Kenya

Ukeketaji

Ni asubuni na mapema,jua linapoanza kuchomoza,katika kijiji kimoja katika Mkoa wa Mashariki.

Kundi la akina mama linafululiza hadi kwa mama mwenzao, huku wakiimba nyimbo za kitamaduni.

Kisa na maana ; hajakeketwa.

Nia yao haswa ni kutumia nguvu kumkeketa kwani ni kero kwa wanawake wa kijiji chao.

Kulingana na mila na desturi ya jamii hiyo ni sharti mwanamke akeketwe anapokaribia kuvunja ungo.Lakini kwa mama Matani* aliolewa kabla hajakeketwa.

La kuhuzunisha ni kwamba yeye ni mjamzito na kitendo hiki kinaweza kuhatarisha maisha yake.

Kwa bahati nzuri,anaepuka gadhabu ya akina mama hao baada ya chifu wa kijiji hicho kuingilia kati.Wanarudi makwao huku wakiapa kumuadhibu mama Matani* baadaye.

Wakati wakujifungua ,yule mama hana budi kuwaita baadhi ya wale wanawake kumsaidia kujifungua.

Sasa wanapata nafasi ya kumkeketa katika ile harakati ya kuzaa.Anajifungua mtoto na afya zake,anakeketwa na sasa ni mama kamili…..unyama ulioje?

 Hii si hadithi bali ndivyo hali ilivyo katika kijiji hicho na kwingineko hapa Kenya.

Kulingana na wataalamu wa afya ukeketaji una adhari chungu nzima.

Madhara yake ni pamoja na kuvuja damu kwa wingi wakati wa kukeketwa,Vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kutokana na ukeketaji kuharibusehemu za uzazi na pia maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi,ugonjwa ambao ni tishio kwa jamii.

Ukeketaji ni mila au desturi potovu ambayo imeshamiri katika baadhi ya majimbo nchini Kenya na pia mataifa ya kanda la Afrika.Mila hii ambayo ni marukufu nchini Kenya,hufanywa hususan msimu wa krismasi.

Kulingana na Mkurungenzi Mtendaji wa Shirika la Idadi ya watu la  Umoja wa Mataifa(UNFPA),nchini Kenya kuna haja ya kuimarisha juhudi ili kukabiliana na ukeketaji.

Akiongea katika hafla ya kuwazawadi waadhishi waliogombea katika maswala ya afya na idadi ya watu jiji Nairobi, alisema mila hii inaweza kutokomeshwa endapo wadau watafanya kampeni kabambe kuwaelimisha wananchi madhara yake .

Zaidi ya watoto wa kike million  tatu wanakeketwa barani Afrika pekee. kulinda haki za watoto wa kike.Nchi hizo ni Ethiopia,Misri,Kenya,Senegal, Bukina faso,Gambia,Guinea na Somalia

Nchini Kenya, mila hii imeshamiri katika  jamii za  wameru,wakisii, waborana, wakuria na wamaasai

Mashirika yasiyo yakiserikali yamekuwa katika nafasi ya kwanza kustumu desturi hiyo ambayo imepitwa na wakati.

Vikundi vya akina mama huko Tigania Mashariki, jimbo la  Meru,vinatoa elimu kwa jamii,ili kulinda haki za mtoto  wa kike.

“Ntanira na mugambo” yaani ni ile hali ya keketa kwa kutumia  maneno kuliko kutumia kisu.Msichana anapobarehe anapewa mafunzo na umuhumu wa kendelea na masomo.

“Hapo awali baadaya ya kukeketwa, msichana aliacha masomo na kuolewa”, anasema mama Kigetu Muthamia aliyekuwa mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake wilayani  Meru.

Ni jambo la kutia moyo kuona kuwa idadi kubwa sasa imekubatia mabadiliko hayo.Kiwango cha ukeketaji nchini Kenya kimeshuka kutoka asilimia 32 hadi asilimia 27, ikilinganishwa na Nchi ya Ethiopia kutoka asilimia 80 hadi 74,huku Misri hali ikiwa ni ya kutamausha kutoka asilimia 97 hadi 81.

Ngariba wengi hapa wamestaafu.Wametupa vifaa vyao vya kazi na kujishughulisha na elimu ya afya inayotolewa na vikundi vya akina mama.

Wanawake wengi wanasema walikuwa wakifanya ukeketaji kwa siri maana walihofia kuandamwa na misimu endapo hawangefuata desturi za jadi.

Juhudi ya kuwaleta pamoja ngariba ,wazee wamila na watoto wa shule pamoja imekuwa ni hatua mwafaka kukomesha ukeketaji.

Kwa hakika serikali haiwezi ikabili tishio hili bila kujumuisha wadai wote,hivyo basi ni jukumu la mashirika ya afya ,ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa hamasa kwa jamii kubadilisha fikra, imani na mitazamo yao kuhusu ukeketaji.












 

 

Alhamisi, 24 Novemba 2011

wakunga wa jadi na uzazi

Wakunga wa jadi na uzazi
Katika kitongoji duni cha Korogocho,kundi la akina mama wajawazito wamepiga foleni wakisubiri kuhudumiwa. Baadhi yao wana uchungu ambao unadhihirika wazi unapowatazama.
wana matumaini watapata afueni punde tu watakapomwona mama ambaye wanamuenzi.
Mama huyu,Jacinta Akinyi, anajulikana kama daktari katika kijiji hiki.Hakika ni kuwa hana elimu yeyote katika taaluma ya udaktari.
Yeye ni mkunga ambaye ana juhudi kama ya mchwa."Daktari" huamka asubuhi na mapema ili kuwahudumia akina mama ambao hawana uwezo wakutafuta matibabu au uchunguzi wanapokuwa katika hali ya ujauzito,katika hospitali za umma.
Gharama ya kujifungua hapa nchini Kenya ni ghari mno,ikilinganishwa na ya wakunga. 

Pia hali ya ukosefu wa usalama katika  mitaa duni ni changamoto kwa mama anayepata uchungu wa kujifungua wakati wa usiku.
Mama Ona ni  baadhi ya akina mama wanaosubiri kujifungua. ingia kwenye chumba ambacho ndani kuna kitanda ambacho kimefichwa na pasia. mkunga akotayari kumuhudumia.
Baada ya nusu saa hivi, kilio cha mtoto inasikika.Mama Ona amejifungua mtoto wa kike.Anasema ana watoto watano ambao kwa usaidizi wa mkunga awewapata.
Bei ya wakunga ni nafuu hapa, ikilinganishwa na bei katika hospitali za kibinafsi au za umma.
Katika hospitali kujifungua ya Pumwani ada ya kujifungua imeongezeka na kufikia shillingi elfu nane huku hospitali kama Nairobi au Aga Khan ada hiyo inaweza ikawa shilling 100,000 kulingana na hali ya mama na mtoto.Endapo mama atafanyiwa upasuaji gharama itakuwa juu zaidi.
Hata hivyo wakunga hukumbana na changamoto chungu nzima.
Mojawapo ni vifo au maradhi yanayosababishwa na:
Uchungu wa mapema na hakuna vifaa vya kuwasaidia.Kutokwa na damu nyingi kabla au baada ya kujifungua.
Wanawake pia wanaweza kupata ugonjwa wa fistula yaani kupasuka kwa mfuko wa uzazi hali ambayo husambabishwa na  uchungu wa muda mrefu,maabukizi ya bacteria kwenye damu au , shinikizo la damu.
Kwa muda mrefu, serikali ya Kenya, imepigia debe umuhimu wa kujifungilia hospitalini.Sababu kuu ikiwa hatari zinazotokana na kujifungulia nyumbani.Na pia ukosefu wa vifaa vya dharula endapo hali ya hatari itatokea mama anapokuwa kwenye ile hali ya kujifungua.
Lakini mfumo wa afya katika vituo umma ya umma, haumushughuliki wanamke ipasavyo.utakuta wanawake zaidi ya kumi wanahudumiwa na muuguzi mmoja,huku mkunga wa kienyeji hutumia muda wakutosha kuhudumia mwanamke mmoja huku akumtuliza hadi ajifungua.
Serikali pia imekuwa ikipendekeza kupigwa marufuku kwa wakunga wa jadi,ambao mara kwa mara hutumia dawa wa kienyeji.
Kuliko kuharamisha shughuli za wakunga wa jadi ni jukumu ya serikali kuboresha huduma zao,ili kupunguza maafa zaidi
Ingawa wanafahami hatari zinazioambatana na ujauzito,mama ona na wenzake hawana nia ya kutafunda usaidizi mahali pengine.
Kulingana na utafiti wa afya uliofanya na serikali mwaka 2011, Kenya ni baadhi ya nchi duniani ambayo ina idadi kubwa ya vifo vya uzazi .
Utafiti pia unaonyesha  asilimia hamsini na saba wanajifungulia majumbani huku asilimia 28 wakisaidiwa na wakunga wa jadi.Pia wanawake wengi wanajifungulia chini ya wakunga wenye ujuzi.Idadi ya wanawake wanaofariki katika sehemu za mashambani ni 608,426.
Huku idadi hii ikiendelea kuongezeka, ni jukumu la serikali kutafuta sera ambazo zitakabiliana na tishio hili, ili kufikia malengo ya millennia ya afya.

Jumanne, 8 Novemba 2011

family planning(uzazi wa mpango)

Aina ya uzazi wa mpango


Kuna  aina za uzazi wa mpango ambazo  mama au baba anaweza kutumia ili kuepuka kupata watoto wasiotarajiwa.


Aina ya uzazi wa mpango

Mpira au kondomu

Kuna kondomu za akina baba na mama pia.
mwanamume anapotumia kondomu inazuia mbegu zake kuingia kwenye mji wa uzazi wa mwanamke.
-Ni rahisi kutumia
-inakinga magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV
-Inazuia mwanamke kupata mimba isiotarajiwa

Shindano(Depo Provera)


Hii njia inafaa kwa mama ambaye hapendi kumeza vidonge na ambaye ameshazaa.
Mwanamke hupata sindano hii ya homoni kila baada ya miezi mitatu.

Hata hivyo mwanamke anapochagua kutumia aina hii ya uzazi wa mpango ni sharti aelewe kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo atakubana nayo kama vile;Kukosa hedhi au kupata hedhi kiasi kidogo.
Pia kuna uwezekano wa kukawia kupata mtoto baada ya kuacha kutumia shindano kwa matarajio ya kutunga mimba.


Vijiti
Hivi ni vijiti vya plastiki vinavyowekwa chini ya ngozi ya mama.vinatolewa kila baada ya miaka mitano.

Hii aina inafaa akina mama ambayo wana watoto na wanataka kupumzika kuzaa kwa muda mrefu.
Kitanzi


Hiki pia ni kifaa cha plastiki ambacho tofauti na vijiti kinakaa kwenye mji wa mimba.
Manufaa
-Inafaa kwa mwanamke aliye na mpenzi mmoja.
-Mbegu za mwanamumu zinazuiwa na kitanzi kukutana na yai la mwanamke.
-Inadumu kwa miaka kumi.
-Punde tu baada ya kutolewa mwanamke anaweza kutunga mimba.
-Inaweza kutolewa wakati wowote.

Adhari
Ni hatari kwa mwanamke aliye na wapenzi wepenzi wengi.

Kufunga kizazi
Hii ni operesheni au upasuaji unaofanywa kuzimba njia ya mayai ya mama au bengu za baba ili zisikutane.

Aina hii inamanufaa kwa mama na baba ambao wana watoto na  hawataraji kuzaa tena.
Pia njia hii haizui kujamiana(tendo la Ndoa)
Isitoshe, namna hii, haina madhara yeyote.

Tembe (vidonge)

Mama humeza kidoge kimoja au viwili kila siku
-Endapo atasahau basi anaweza akapata ujauzito.
-Haizui magonjwa ya zinaa .
-Mama pia anahitaji kupimwa shinikizo la damu mara kwa mara.

La muhimu ni kujua kuwa aina hizi haizui mtu kupata magonjwa ya zinaa.

population (idadi ya watu)

Huku idadi ya watu ikifikia billioni 7 duniani, kuna haja ya kuudwa kwa mikakati mwafaka, ili kukabiliana na changamoto zinazoabatana na ongezeko la watu.

 Kulingana na takwimu zilizotolewa na umoja wa mataifa, idadi ya watu, inakadiriwa kuongezeka hadi billioni 9 ifikapo mwaka wa 2050.

Barani Afrika hivi sasa idadi imefika billioni moja na inatarajiwa kuongezeka marudufu ifikapo 2050.

Zaidi ya hayo, Bara la Afrika lina kibarua kigumu kutafuta shuluhu la haraka na la kudumu  ili kuhakikisha idadi ya  watu imedhibitiwa.

Umaskini, uhaba wa vituo vya afya,upungufu wa madawa ni baadhi tu ya changamoto nyingi ambazo zimeendelea kuwa tishio.

Ili kufikia malengo ya milenia ya afya sharti maswala ya elimu, matibabu(afya), usalama wa chakula na ajira yatiliwe maanani.

Baadhi ya suluhu ni kuimarisha kampeni ya uzazi wa mpango.Hata hiyo kampeni hizo zisiwalenge pekee akina mama bali akina baba wahusishwe pia.

Kwa muda mrefu mwanamke ndiye anayelengwa na uzazi wa mpango huku mwanamume akitengwa.Kufuatia hali hiyo, wanamume wengi huwakataza wake zao kutafuta elimu ya uzazi wa mpango.
Pia desturi na tamaduni za kiafrika na kidini zinachangia ongezeko la watu.

Hata hivyo kuna nchi ambazo zinajizatiti kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya afya ya uzazi.
Nchini ya Kenya umetilia maanani uzazi wa mpango na inaendeleza kampeni hizo kupitia kwa vyombo vya habari, wahudumu wa afya na pia katika vituo vya afya.

Nchi ya Rwanda pia inatilia mkazo uzazi wa mpango,huku sera ya uzazi wa mpango ikisizitisha  kila familia kuzaa watoto watatu.

Mwezi huu wa Novemba, kutakuwa na kongamano kuhusu uzazi wa mpango  Mjini Dakar, Senegal .Kongamano hilo litawajumuisha  wadau katika sekta ya afya.
Uzazi wa mpango na afya ya kizazi ni baadhi tu ya maswala  yatakayojadiliwa.

Ijumaa, 4 Novemba 2011

shindano ya homoni ya depo provera

Uzazi wa mpango
Ni ile hali ya mume na mkewe kukumbaliana jinzi au namna ya kupunguza mimba zisizotarajiwa.

Serikali ya kenya imetilia mkazo umuhimu uzazi wa mpango.Zaidi ya hayo, kuna namna  na aina tofauti za uzazi wa mpango.

Kuna vidonge vya kumeza, shindano ijulikanayo kama Depo provera, Vijiti, kitanzi, mpira wa mama au baba,kufunga kizazi kwa mama au baba na njia za asili.


Ukweli ni kuwa, ni mpira pekee kati ya  aina zote za mpango wa uzazi inayozuia maambukizi ya ugonjwa. Aina zinginezo hazizui kupata magonjwa ya zinaa na pia virusi vya ukimwi.

Bali na hayo, kuna dhana potofu kwa baadhi ya watu  wanaoamini kuwa matumishi ya auna hizi zote za uzazi wa mpango zinazuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi ya ukimwi.

Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika moja la afya la Marekani na kuchapishwa na jarida la The Lancet, akina mama wanaotumia aina hii ya upangaji uzazi wako  hatarini ya kuambukizwa au kuwaambukiza waume wao virusi vya HIV,kuliko wale wasiotumia aina hii.

Uvumbuzi kuwa utumiaji dawa ya upangaji uzazi ya homoni ijulikanayo kama devo provera unachangia ongezeko la maabukuzi ya ugonjwa hatari wa ukimwi umetia wengi kiwewe.Inakisiwa takribani millioni 12 ya wanawake wenye umri wa kati ya  miaka 15 na 49 katika Afrika kusini na Jangwa la Sahara wanatumia homoni za kuzuia mimba(Depo provera).

Takwimu pia sinaonyesha kuwa kuna zaidi ya wanawake milioni 140 duniani kote wanaotumia njia ya homoni za uzazi wa mpango.

Kulingana na Daktari Joseph Karanja ambaye ni mtaalamu wa afya ya uzazi,kuna haja ya kutumia aina  mbili za uzazi wa mpango,hususan kwa watu walio hatarini ya kuambukizwa virusi vya HIV.

Dkt Karanja anasisitiza kuwa ni muhimu kutumia kondomu au mpira wa mama au babana na dawa za hononi kwa pamoja ili kujikinga kutokana na makali ya ukimwi.

Mkurungenzi wa afya ya umma  nchini Kenya Dkt.Shariff Shahnaz aliwataka wakenya wasiwe na hofu kwani  serikali inachunguza kwa makini matokeo hao.
Alisema hivi karibuni,serikali itatoa msimamo wake kuhusu dawa ya homoni ya uzazi wa mpango(depo provera).

Kufuatia utafiti huu,Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha mkutano Januari mwaka ujao(2012) ili kutadhimini iwapo ushahidi huu unatosha kuwashauri wanawake kuachana na aina hii ya mpango wa uzazi ili kukomesha maambukizi zaidi.

Huu ni mjadala ambao umetia wengi hofu ,kwani wanamke ambaye ameolewa hawawezi kusurutisha waume zao kutumia kondomu wanapofanya tendo la ndoa nao,au wao kutumia mpira.

Uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya wanaume hawakubariani na uzazi wa mpango.
Hii itakuwa ni changamoto kwa mke na mume kuzungumzia swala hili, ili kuwe na afya bora na pia kupata watoto wanaoweza kuwalea.

Pia itakuwa muhimu, kwa kuboresha afya ya  mama na mtoto.

Utafiti huu wa  multicentre ulifanywa katika nchi saba za Afrika. Botswana, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda na Zimbabwe.Wanandoa 3,000 walihusishwa.

Fauka ya hayo, utafiti huo ulibainisha kuwa wanawake wanaotumia dawa hizo huambukizwa virusi ya Ukimwi kwa 6.61 kwa kila watu 100, ikilinganishwa na watu 3.78 wasiotumia dawa hizo.

Inaaminika kuwa zaidi ya asili mia 39 % ya wanawake nchini kenya walioko kwenye ndoa wanatumia aina hii ya Devo provera kupanga uzazi.