Wakunga wa jadi na uzazi
Katika kitongoji duni cha Korogocho,kundi la akina mama wajawazito wamepiga foleni wakisubiri kuhudumiwa. Baadhi yao wana uchungu ambao unadhihirika wazi unapowatazama.
wana matumaini watapata afueni punde tu watakapomwona mama ambaye wanamuenzi.
Mama huyu,Jacinta Akinyi, anajulikana kama daktari katika kijiji hiki.Hakika ni kuwa hana elimu yeyote katika taaluma ya udaktari.
Yeye ni mkunga ambaye ana juhudi kama ya mchwa."Daktari" huamka asubuhi na mapema ili kuwahudumia akina mama ambao hawana uwezo wakutafuta matibabu au uchunguzi wanapokuwa katika hali ya ujauzito,katika hospitali za umma.
Gharama ya kujifungua hapa nchini Kenya ni ghari mno,ikilinganishwa na ya wakunga.
Pia hali ya ukosefu wa usalama katika mitaa duni ni changamoto kwa mama anayepata uchungu wa kujifungua wakati wa usiku.
Pia hali ya ukosefu wa usalama katika mitaa duni ni changamoto kwa mama anayepata uchungu wa kujifungua wakati wa usiku.
Mama Ona ni baadhi ya akina mama wanaosubiri kujifungua. ingia kwenye chumba ambacho ndani kuna kitanda ambacho kimefichwa na pasia. mkunga akotayari kumuhudumia.
Baada ya nusu saa hivi, kilio cha mtoto inasikika.Mama Ona amejifungua mtoto wa kike.Anasema ana watoto watano ambao kwa usaidizi wa mkunga awewapata.
Bei ya wakunga ni nafuu hapa, ikilinganishwa na bei katika hospitali za kibinafsi au za umma.
Katika hospitali kujifungua ya Pumwani ada ya kujifungua imeongezeka na kufikia shillingi elfu nane huku hospitali kama Nairobi au Aga Khan ada hiyo inaweza ikawa shilling 100,000 kulingana na hali ya mama na mtoto.Endapo mama atafanyiwa upasuaji gharama itakuwa juu zaidi.
Hata hivyo wakunga hukumbana na changamoto chungu nzima.
Mojawapo ni vifo au maradhi yanayosababishwa na:
Uchungu wa mapema na hakuna vifaa vya kuwasaidia.Kutokwa na damu nyingi kabla au baada ya kujifungua.
Wanawake pia wanaweza kupata ugonjwa wa fistula yaani kupasuka kwa mfuko wa uzazi hali ambayo husambabishwa na uchungu wa muda mrefu,maabukizi ya bacteria kwenye damu au , shinikizo la damu.
Kwa muda mrefu, serikali ya Kenya, imepigia debe umuhimu wa kujifungilia hospitalini.Sababu kuu ikiwa hatari zinazotokana na kujifungulia nyumbani.Na pia ukosefu wa vifaa vya dharula endapo hali ya hatari itatokea mama anapokuwa kwenye ile hali ya kujifungua.
Lakini mfumo wa afya katika vituo umma ya umma, haumushughuliki wanamke ipasavyo.utakuta wanawake zaidi ya kumi wanahudumiwa na muuguzi mmoja,huku mkunga wa kienyeji hutumia muda wakutosha kuhudumia mwanamke mmoja huku akumtuliza hadi ajifungua.
Serikali pia imekuwa ikipendekeza kupigwa marufuku kwa wakunga wa jadi,ambao mara kwa mara hutumia dawa wa kienyeji.
Kuliko kuharamisha shughuli za wakunga wa jadi ni jukumu ya serikali kuboresha huduma zao,ili kupunguza maafa zaidi
Ingawa wanafahami hatari zinazioambatana na ujauzito,mama ona na wenzake hawana nia ya kutafunda usaidizi mahali pengine.
Kulingana na utafiti wa afya uliofanya na serikali mwaka 2011, Kenya ni baadhi ya nchi duniani ambayo ina idadi kubwa ya vifo vya uzazi .
Utafiti pia unaonyesha asilimia hamsini na saba wanajifungulia majumbani huku asilimia 28 wakisaidiwa na wakunga wa jadi.Pia wanawake wengi wanajifungulia chini ya wakunga wenye ujuzi.Idadi ya wanawake wanaofariki katika sehemu za mashambani ni 608,426.
Huku idadi hii ikiendelea kuongezeka, ni jukumu la serikali kutafuta sera ambazo zitakabiliana na tishio hili, ili kufikia malengo ya millennia ya afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni