Uzazi wa mpango
Ni ile hali ya mume na mkewe kukumbaliana jinzi au namna ya kupunguza mimba zisizotarajiwa.
Serikali ya kenya imetilia mkazo umuhimu uzazi wa mpango.Zaidi ya hayo, kuna namna na aina tofauti za uzazi wa mpango.
Kuna vidonge vya kumeza, shindano ijulikanayo kama Depo provera, Vijiti, kitanzi, mpira wa mama au baba,kufunga kizazi kwa mama au baba na njia za asili.
Ukweli ni kuwa, ni mpira pekee kati ya aina zote za mpango wa uzazi inayozuia maambukizi ya ugonjwa. Aina zinginezo hazizui kupata magonjwa ya zinaa na pia virusi vya ukimwi.
Bali na hayo, kuna dhana potofu kwa baadhi ya watu wanaoamini kuwa matumishi ya auna hizi zote za uzazi wa mpango zinazuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi ya ukimwi.
Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika moja la afya la Marekani na kuchapishwa na jarida la The Lancet, akina mama wanaotumia aina hii ya upangaji uzazi wako hatarini ya kuambukizwa au kuwaambukiza waume wao virusi vya HIV,kuliko wale wasiotumia aina hii.
Uvumbuzi kuwa utumiaji dawa ya upangaji uzazi ya homoni ijulikanayo kama devo provera unachangia ongezeko la maabukuzi ya ugonjwa hatari wa ukimwi umetia wengi kiwewe.Inakisiwa takribani millioni 12 ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 katika Afrika kusini na Jangwa la Sahara wanatumia homoni za kuzuia mimba(Depo provera).
Takwimu pia sinaonyesha kuwa kuna zaidi ya wanawake milioni 140 duniani kote wanaotumia njia ya homoni za uzazi wa mpango.
Kulingana na Daktari Joseph Karanja ambaye ni mtaalamu wa afya ya uzazi,kuna haja ya kutumia aina mbili za uzazi wa mpango,hususan kwa watu walio hatarini ya kuambukizwa virusi vya HIV.
Dkt Karanja anasisitiza kuwa ni muhimu kutumia kondomu au mpira wa mama au babana na dawa za hononi kwa pamoja ili kujikinga kutokana na makali ya ukimwi.
Mkurungenzi wa afya ya umma nchini Kenya Dkt.Shariff Shahnaz aliwataka wakenya wasiwe na hofu kwani serikali inachunguza kwa makini matokeo hao.
Alisema hivi karibuni,serikali itatoa msimamo wake kuhusu dawa ya homoni ya uzazi wa mpango(depo provera).
Kufuatia utafiti huu,Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha mkutano Januari mwaka ujao(2012) ili kutadhimini iwapo ushahidi huu unatosha kuwashauri wanawake kuachana na aina hii ya mpango wa uzazi ili kukomesha maambukizi zaidi.
Huu ni mjadala ambao umetia wengi hofu ,kwani wanamke ambaye ameolewa hawawezi kusurutisha waume zao kutumia kondomu wanapofanya tendo la ndoa nao,au wao kutumia mpira.
Uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya wanaume hawakubariani na uzazi wa mpango.
Hii itakuwa ni changamoto kwa mke na mume kuzungumzia swala hili, ili kuwe na afya bora na pia kupata watoto wanaoweza kuwalea.
Pia itakuwa muhimu, kwa kuboresha afya ya mama na mtoto.
Utafiti huu wa multicentre ulifanywa katika nchi saba za Afrika. Botswana, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda na Zimbabwe.Wanandoa 3,000 walihusishwa.
Fauka ya hayo, utafiti huo ulibainisha kuwa wanawake wanaotumia dawa hizo huambukizwa virusi ya Ukimwi kwa 6.61 kwa kila watu 100, ikilinganishwa na watu 3.78 wasiotumia dawa hizo.
Inaaminika kuwa zaidi ya asili mia 39 % ya wanawake nchini kenya walioko kwenye ndoa wanatumia aina hii ya Devo provera kupanga uzazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni