FGM (ukeketaji) Kenya
Ukeketaji
Ni asubuni na mapema,jua linapoanza kuchomoza,katika kijiji kimoja katika Mkoa wa Mashariki.
Kundi la akina mama linafululiza hadi kwa mama mwenzao, huku wakiimba nyimbo za kitamaduni.
Kisa na maana ; hajakeketwa.
Nia yao haswa ni kutumia nguvu kumkeketa kwani ni kero kwa wanawake wa kijiji chao.
Kulingana na mila na desturi ya jamii hiyo ni sharti mwanamke akeketwe anapokaribia kuvunja ungo.Lakini kwa mama Matani* aliolewa kabla hajakeketwa.
La kuhuzunisha ni kwamba yeye ni mjamzito na kitendo hiki kinaweza kuhatarisha maisha yake.
Kwa bahati nzuri,anaepuka gadhabu ya akina mama hao baada ya chifu wa kijiji hicho kuingilia kati.Wanarudi makwao huku wakiapa kumuadhibu mama Matani* baadaye.
Wakati wakujifungua ,yule mama hana budi kuwaita baadhi ya wale wanawake kumsaidia kujifungua.
Sasa wanapata nafasi ya kumkeketa katika ile harakati ya kuzaa.Anajifungua mtoto na afya zake,anakeketwa na sasa ni mama kamili…..unyama ulioje?
Hii si hadithi bali ndivyo hali ilivyo katika kijiji hicho na kwingineko hapa Kenya.
Kulingana na wataalamu wa afya ukeketaji una adhari chungu nzima.
Madhara yake ni pamoja na kuvuja damu kwa wingi wakati wa kukeketwa,Vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kutokana na ukeketaji kuharibusehemu za uzazi na pia maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi,ugonjwa ambao ni tishio kwa jamii.
Ukeketaji ni mila au desturi potovu ambayo imeshamiri katika baadhi ya majimbo nchini Kenya na pia mataifa ya kanda la Afrika.Mila hii ambayo ni marukufu nchini Kenya,hufanywa hususan msimu wa krismasi.
Kulingana na Mkurungenzi Mtendaji wa Shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa(UNFPA),nchini Kenya kuna haja ya kuimarisha juhudi ili kukabiliana na ukeketaji.
Akiongea katika hafla ya kuwazawadi waadhishi waliogombea katika maswala ya afya na idadi ya watu jiji Nairobi, alisema mila hii inaweza kutokomeshwa endapo wadau watafanya kampeni kabambe kuwaelimisha wananchi madhara yake .
Zaidi ya watoto wa kike million tatu wanakeketwa barani Afrika pekee. kulinda haki za watoto wa kike.Nchi hizo ni Ethiopia,Misri,Kenya,Senegal, Bukina faso,Gambia,Guinea na Somalia
Nchini Kenya, mila hii imeshamiri katika jamii za wameru,wakisii, waborana, wakuria na wamaasai
Mashirika yasiyo yakiserikali yamekuwa katika nafasi ya kwanza kustumu desturi hiyo ambayo imepitwa na wakati.
Vikundi vya akina mama huko Tigania Mashariki, jimbo la Meru,vinatoa elimu kwa jamii,ili kulinda haki za mtoto wa kike.
“Ntanira na mugambo” yaani ni ile hali ya keketa kwa kutumia maneno kuliko kutumia kisu.Msichana anapobarehe anapewa mafunzo na umuhumu wa kendelea na masomo.
“Hapo awali baadaya ya kukeketwa, msichana aliacha masomo na kuolewa”, anasema mama Kigetu Muthamia aliyekuwa mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake wilayani Meru.
Ni jambo la kutia moyo kuona kuwa idadi kubwa sasa imekubatia mabadiliko hayo.Kiwango cha ukeketaji nchini Kenya kimeshuka kutoka asilimia 32 hadi asilimia 27, ikilinganishwa na Nchi ya Ethiopia kutoka asilimia 80 hadi 74,huku Misri hali ikiwa ni ya kutamausha kutoka asilimia 97 hadi 81.
Ngariba wengi hapa wamestaafu.Wametupa vifaa vyao vya kazi na kujishughulisha na elimu ya afya inayotolewa na vikundi vya akina mama.
Wanawake wengi wanasema walikuwa wakifanya ukeketaji kwa siri maana walihofia kuandamwa na misimu endapo hawangefuata desturi za jadi.
Juhudi ya kuwaleta pamoja ngariba ,wazee wamila na watoto wa shule pamoja imekuwa ni hatua mwafaka kukomesha ukeketaji.
Kwa hakika serikali haiwezi ikabili tishio hili bila kujumuisha wadai wote,hivyo basi ni jukumu la mashirika ya afya ,ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa hamasa kwa jamii kubadilisha fikra, imani na mitazamo yao kuhusu ukeketaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni