Mkutano huu unafanyika huku karibu watu millioni 900 kote duniani wakikumbatia uzazi wa mpango.
Hata hivyo, sio wote wanaoweza kufanya uzazi wa mpango wakati wanapotaka kufuatia changamoto kadha wa kadha.
Mkutano huu utawajumuisha watafiti wa afya,madaktari na wadau wengine katika sekta ya afya.
Kufanyika kwa mkutano huu katika Afrika Magharibi,ni jambo la muhimu ikifahamika kuwa nchi za Afrika Magharibi zinaongoza kwa idadi ya watu kwani mpango wa uzazi ungali haujapewa kipao mbele.
Pia kupata hutuma ya uzazi wa mpango ni shinda.
Inaaminika kuwa wazazi wengi ambao wangependa kupanga uzazi wanasubuka sana.Hata kabla wapate huduma hiyo muhimu wanagundua kuwa ni wajawazito.Idadi ya wanandoa walio kwenye hali hii ni zaidi ya millioni 215 kote duniani.
Uzazi wa mpango unawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya ya familia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni