Huku idadi ya watu ikifikia billioni 7 duniani, kuna haja ya kuudwa kwa mikakati mwafaka, ili kukabiliana na changamoto zinazoabatana na ongezeko la watu.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na umoja wa mataifa, idadi ya watu, inakadiriwa kuongezeka hadi billioni 9 ifikapo mwaka wa 2050.
Barani Afrika hivi sasa idadi imefika billioni moja na inatarajiwa kuongezeka marudufu ifikapo 2050.
Zaidi ya hayo, Bara la Afrika lina kibarua kigumu kutafuta shuluhu la haraka na la kudumu ili kuhakikisha idadi ya watu imedhibitiwa.
Umaskini, uhaba wa vituo vya afya,upungufu wa madawa ni baadhi tu ya changamoto nyingi ambazo zimeendelea kuwa tishio.
Baadhi ya suluhu ni kuimarisha kampeni ya uzazi wa mpango.Hata hiyo kampeni hizo zisiwalenge pekee akina mama bali akina baba wahusishwe pia.
Kwa muda mrefu mwanamke ndiye anayelengwa na uzazi wa mpango huku mwanamume akitengwa.Kufuatia hali hiyo, wanamume wengi huwakataza wake zao kutafuta elimu ya uzazi wa mpango.
Pia desturi na tamaduni za kiafrika na kidini zinachangia ongezeko la watu.
Hata hivyo kuna nchi ambazo zinajizatiti kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya afya ya uzazi.
Nchini ya Kenya umetilia maanani uzazi wa mpango na inaendeleza kampeni hizo kupitia kwa vyombo vya habari, wahudumu wa afya na pia katika vituo vya afya.
Nchi ya Rwanda pia inatilia mkazo uzazi wa mpango,huku sera ya uzazi wa mpango ikisizitisha kila familia kuzaa watoto watatu.
Mwezi huu wa Novemba, kutakuwa na kongamano kuhusu uzazi wa mpango Mjini Dakar, Senegal .Kongamano hilo litawajumuisha wadau katika sekta ya afya.
Uzazi wa mpango na afya ya kizazi ni baadhi tu ya maswala yatakayojadiliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni