Jumapili, 29 Julai 2012

Waziri wa afya ya umma Beth Mugo apona kansa.ugonjwa wa kanza ume kuwa tishio hapa nchini Kenya na pia mataifa mengi ya Afrika.

hata hivyo kulingana na waziri beth Mugo ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa na kupoona endapo utagunduliwa mapema.


Akizungumza jana baadha ya kuasiri kutoka Marekani ambako amekuewa akipokea matibabu ya kansa, waziri Mugo ametangaza kuwa kenya itafungua kituo cha Kansa nchini ilikuwatibu watu wanaougua ugonjwa huo.
Bi mugo aligunduliwa kuugua kanza ya matiti na kwa bahati nzuri iligunduliwa kabla haijaenea na kwa sasa anasema ako salama salimini.

Pia waziri mugo alionya wakenya kuhakikisha kuwa wanaishi kwenye mazingira safi, kwani uhalibifu wa mazingira hunachangia kuenea kwa ugonjwa hatari wa kansa.

"Hewa safi, mazingira mema na lishe bora ni muhimu kwa kuepa maradhi ya kansa.
Ni jukumu letu kama wakenya kudumisha usafi na pia upanzi wa miti ili kupata hewa safi.Hii itakuwa ni njia moja ya kuepuka maradhi hatari ya kansa.

Hivi majuzi rais Mwai kibaki aliidhinisha mswada wa kansa nchini,hii inapika hatua kupwa ya kukabiliana na ugonjwa huu.

matibabu ya kasa hapa nchini yamekuwa wa changamoto kadha wa kadha; kama vile ukosefu wa vifaa vya ukaguzi wa saratani, kampeni ya kuwafahamisha wananchi madhara na dalili za saratani,ghalama ya juu ya kutibu ugonjwa huu baadhi ya matatizo mengine.

Sadifa ni kuwa waziri wa afya ya umma na mwenzake wa humuda za afya Anyang Nyongo wamekuwa wakiugua saratani lakini wote wamepona, baada ya kupokea matibabu marekani.

Baadhi ya saratani ambayo inaadhiri wa kenya wa kike ni;saratani ya sehemu ya uzazi na ile ya matiti, huku wanaume wakiugua saratani ya koo na ya prostate.

Endapo serikali itachukua jukumu ya kutafuta yamna ya kukomesha kuenea kwa saratani hapa nchini ,itakuwa afueni kwa wananchi ambao gharama ya matibabu imekuwa ni ghali mno hadi wanaamua kutotafuta matibabu.


Baadhi ya wanakenya mashuhuri wanaugua saratani ni aliyekuwa mbunge wa Butere bwana martin shikuku.Tunamuombea afueni ya haraka,


Jumatano, 18 Julai 2012

Tohara-Ujeremani


Utata kuhusu tohara ya wanaume imetatuliwa baada ya Kansela wa Ujerumani kuunga mkono jamii za Kiyaudi na za Kiislaamu zinazo taka kitendo cha kutahiriwa kiendelee katika jamii zao.


Mseamji wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert alisema " kutailiwa kwa watoto wa kiume ni kitendo ambacho kinakwenda sambamba na imani ya dini hizo na hakuna adhabu itakayo tolewa.

"Na ieleweke serikali inaruhusu haki ya kiimani na Wayahudi na Waislaam ni Wajeruamani hivyo wanahaki sawa na Wajerumani wangine."

Kuungwa mkuno huko kwa kitendo cha kutailiwa kumekuja baaada ya daktari mmoja kutokutwa na hatia ya kusababisha maumivu kwa mtoto aliye mtairi, ambapo ilidaiwa mtoto huyo alikutwa na matatizo ya kiafya kutokana kutailiwa huko.

Hata hivyo kitendo cha kutailiwa kimekuwa kinaleta mvutano katika jamii nchi Ujerumani huku wengine wakipinga na wengine wakiunga mkono.

Tohara ya mwanaume ni ile hali ya ukataji wa ngozi ya mbele inayoficha kichwa cha uume.Kulingana na wataalamu wa afya mwanamke ambaye mumewe ametailiwa ana uwezekano mdogo wa kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.Tohara ufanywa kwa sababu mbalimbali;za kidini kitamaduni,kiafya na kwa sababu za kudumisha usafi.

 


kongamano la afya ya uzazi London


Katika juhudi zake za kuboresha sera za uzazi , jumuia ya kimataifa  imeada mkutano wa kujadili uzazi wa mpango nchini  Ungereza.

Mkutano huu wa kimataifa utajadili Uzazi wa Mpango kwa nchi maskini zaidi duniani.

Baadhi ya viongozi wa Afrika walioalikwa kwenye  mkutano huu ni pamoja na ; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete , Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Mwenyeji wa mkutano huu ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroun.

Mkutano ,huu wa siku moja umedhaminiwa na Serikali ya Uingereza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Taasisi ya Bill and Belinda Gates Foundation.

Ni mara ya kwanza mkutano wa aina hii unafanyika nchini Uingereza ,na utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Queen Elizabeth.

Inakisiwa  utaanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

Isitoshe, mkutano huo ni nafasi ya pamoja ya kuiwezesha jumuia ya kimataifa kuonyesha dhamira zaidi katika huduma za uzazi bora ambazo kwa kiasi fulani zitachangia kuongeza kasi katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia nambari nne  kupunguza vifo vya watoto  na nambari tano kuboresha afya za akinamama.

Inakadiriwa kuwa zitahitaji kiasi cha dola za Marekani bilioni 10 kwa miaka minane ijayo kuanzia sasa 2012 hadi 2020 ili kudumisha huduma za sasa za uzazi bora duniani. Kiasi cha dola bilioni nne za ziada zitahitaji ili kuweza kuwafikisha wanawake milioni 120 katika nchi masikini zaidi ambao kwa sasa hawapati huduma hizo katika miaka hiyo minane ijayo.

Alhamisi, 5 Julai 2012

Arafat

Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat watoa majibu nusu.


marehemu Arafat wakati akiwa mwenye afya nzuri

marehemu Arafat baada ya kuugua
 
 Uchunguzi wa kisayansi uliyofanywa kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi na rais wa Wapalestina umetoa majibu nusu tangu kuanza kwa uchunguzi huo.
Rais Yasir Arafat ambaye alifariki dunia nchini Ufaransa ambapo alipelekwa kwa ajili yamatibabu baada ya kuugua wakati akiwa amefungiwa  kutoka katika mji wa Ramallah na serikali Izrael.
 
Dr Francois Bochud ambaye ni mtaalamu wa Radiophysique iliyopo nchini Switzerland alisema " naweza kusema tumekuta aina ya gesi inayo julikana kama polonium-210 ambayo inaweza kuwa chanzo ca kifo chake na tunaweza kupata jibu sahihi ikiwa baadhi ya viungo vya marehemu Yasir Arafat vitapatikana kwa  uchunguzi zaidi."
 
Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat ulikuja baada ya mkewe Suha Arafat  kuruhusu uchunguzi kuendelea na kutoa ruhusa ya kuwa mwili wa Yasir Araf ufukuliwe kwa uchunguzi zaidi  na kuiomba serikali ya Wapalestina kushirikiana naye.

Wasifu wa arafat
Alikuwa kiongozi shupavu wa Palestina  aliyeenziwa na wale alioongoza.