Jumatano, 18 Julai 2012

Tohara-Ujeremani


Utata kuhusu tohara ya wanaume imetatuliwa baada ya Kansela wa Ujerumani kuunga mkono jamii za Kiyaudi na za Kiislaamu zinazo taka kitendo cha kutahiriwa kiendelee katika jamii zao.


Mseamji wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert alisema " kutailiwa kwa watoto wa kiume ni kitendo ambacho kinakwenda sambamba na imani ya dini hizo na hakuna adhabu itakayo tolewa.

"Na ieleweke serikali inaruhusu haki ya kiimani na Wayahudi na Waislaam ni Wajeruamani hivyo wanahaki sawa na Wajerumani wangine."

Kuungwa mkuno huko kwa kitendo cha kutailiwa kumekuja baaada ya daktari mmoja kutokutwa na hatia ya kusababisha maumivu kwa mtoto aliye mtairi, ambapo ilidaiwa mtoto huyo alikutwa na matatizo ya kiafya kutokana kutailiwa huko.

Hata hivyo kitendo cha kutailiwa kimekuwa kinaleta mvutano katika jamii nchi Ujerumani huku wengine wakipinga na wengine wakiunga mkono.

Tohara ya mwanaume ni ile hali ya ukataji wa ngozi ya mbele inayoficha kichwa cha uume.Kulingana na wataalamu wa afya mwanamke ambaye mumewe ametailiwa ana uwezekano mdogo wa kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.Tohara ufanywa kwa sababu mbalimbali;za kidini kitamaduni,kiafya na kwa sababu za kudumisha usafi.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni