Katika juhudi zake za kuboresha sera za uzazi , jumuia ya kimataifa imeada mkutano wa kujadili uzazi wa mpango nchini Ungereza.
Mkutano huu wa kimataifa utajadili Uzazi wa Mpango kwa nchi maskini zaidi duniani.
Baadhi ya viongozi wa Afrika walioalikwa kwenye mkutano huu ni pamoja na ; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete , Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Mwenyeji wa mkutano huu ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroun.
Mkutano ,huu wa siku moja umedhaminiwa na Serikali ya Uingereza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Taasisi ya Bill and Belinda Gates Foundation.
Ni mara ya kwanza mkutano wa aina hii unafanyika nchini Uingereza ,na utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Queen Elizabeth.
Inakisiwa utaanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Isitoshe, mkutano huo ni nafasi ya pamoja ya kuiwezesha jumuia ya kimataifa kuonyesha dhamira zaidi katika huduma za uzazi bora ambazo kwa kiasi fulani zitachangia kuongeza kasi katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia nambari nne kupunguza vifo vya watoto na nambari tano kuboresha afya za akinamama.
Inakadiriwa kuwa zitahitaji kiasi cha dola za Marekani bilioni 10 kwa miaka minane ijayo kuanzia sasa 2012 hadi 2020 ili kudumisha huduma za sasa za uzazi bora duniani. Kiasi cha dola bilioni nne za ziada zitahitaji ili kuweza kuwafikisha wanawake milioni 120 katika nchi masikini zaidi ambao kwa sasa hawapati huduma hizo katika miaka hiyo minane ijayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni