Jumapili, 29 Julai 2012

Waziri wa afya ya umma Beth Mugo apona kansa.ugonjwa wa kanza ume kuwa tishio hapa nchini Kenya na pia mataifa mengi ya Afrika.

hata hivyo kulingana na waziri beth Mugo ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa na kupoona endapo utagunduliwa mapema.


Akizungumza jana baadha ya kuasiri kutoka Marekani ambako amekuewa akipokea matibabu ya kansa, waziri Mugo ametangaza kuwa kenya itafungua kituo cha Kansa nchini ilikuwatibu watu wanaougua ugonjwa huo.
Bi mugo aligunduliwa kuugua kanza ya matiti na kwa bahati nzuri iligunduliwa kabla haijaenea na kwa sasa anasema ako salama salimini.

Pia waziri mugo alionya wakenya kuhakikisha kuwa wanaishi kwenye mazingira safi, kwani uhalibifu wa mazingira hunachangia kuenea kwa ugonjwa hatari wa kansa.

"Hewa safi, mazingira mema na lishe bora ni muhimu kwa kuepa maradhi ya kansa.
Ni jukumu letu kama wakenya kudumisha usafi na pia upanzi wa miti ili kupata hewa safi.Hii itakuwa ni njia moja ya kuepuka maradhi hatari ya kansa.

Hivi majuzi rais Mwai kibaki aliidhinisha mswada wa kansa nchini,hii inapika hatua kupwa ya kukabiliana na ugonjwa huu.

matibabu ya kasa hapa nchini yamekuwa wa changamoto kadha wa kadha; kama vile ukosefu wa vifaa vya ukaguzi wa saratani, kampeni ya kuwafahamisha wananchi madhara na dalili za saratani,ghalama ya juu ya kutibu ugonjwa huu baadhi ya matatizo mengine.

Sadifa ni kuwa waziri wa afya ya umma na mwenzake wa humuda za afya Anyang Nyongo wamekuwa wakiugua saratani lakini wote wamepona, baada ya kupokea matibabu marekani.

Baadhi ya saratani ambayo inaadhiri wa kenya wa kike ni;saratani ya sehemu ya uzazi na ile ya matiti, huku wanaume wakiugua saratani ya koo na ya prostate.

Endapo serikali itachukua jukumu ya kutafuta yamna ya kukomesha kuenea kwa saratani hapa nchini ,itakuwa afueni kwa wananchi ambao gharama ya matibabu imekuwa ni ghali mno hadi wanaamua kutotafuta matibabu.


Baadhi ya wanakenya mashuhuri wanaugua saratani ni aliyekuwa mbunge wa Butere bwana martin shikuku.Tunamuombea afueni ya haraka,


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni