Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2012

WHO Malaria Kenya

Picha
Kenya yatoa ripoti zisizo kamili Serikali ya Kenya imepiga hatua kukabiliana na ugonjwa wa malaria,ingawa hatua zake hazijaridhisha Shirika la Afya Duniani. Kulingana na ripoti iliyotolewa rasmi na Shirika la Afya Duniani(WHO),tathmini ya maendeleo ya Kenya kupambana na malaria haiwezi kufanywa kwa sababu takwimu zake si kamili kudhibitisha juhudi zake za kuukabili ugonjwa wa malaria. WHO imetaja Kenya kuwa miongoni mwa nchi saba katika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambazo viwango vya maambukizi vingali juu,huku huduma za afya zikiwa mbali na wananchi. Zaidi ya hayo, serikali ya Kenya ilitoa ripoti kudhibitisha kutumia Dollar za Marekani 2,700,000 katika mipango yake ya kupambana na malaria katika mwaka 2010.Hata hivyo hakuna takwimu zinapatikana ama zilizotolewa katika kipindi za  2011. Katika kipindi za 2010 Kenya ilipata Dollar za Marekani 39,100,000 kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa iliyofadhiliwa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi , K...

Mandela hospitali

Picha
  Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea kupokea matibabu hospitali mjini Pretoria ambako anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu. Mzee Mandela alipelekwa na kulazwa hospitali, Jumamosi(wiki moja iliyopita). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea, Mandela naendelea kupata nafuu. Mapema mwaka huu, Mandela alilazwa hospitali ili kutibiwa matatizo ya tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu. Homa ya mapafu, husababishwa na viini tete vijulikanavyo kama (Streptococcus pneumoniae) na huathiri sehemu za kupumua kwenye mapafu . Bwana Mandela amewahi kutibiwa kwa mara nyingine ugojwa wa kifua kikuu unaoathiri mapafu. Magonjwa mengi ya mapafu hutibiwa kwa madawa , mgonjwa kupu mzika au kupata vinywaji vingi.     Wazee na watu ambaom hawakinga ya mwili ndiyo huadhiriwa na maradhi haya. Bwana Mandela ana miaka 94.

mkataba wa Kyoto

Picha
  Hatimaye mkutano wa kujadili mabadiliko ya hali ya hewa mjini Doha umeafiki kurefushwa Mkataba wa Kyoto hata baada ya   nchi ya   Urusi kujaribu kuyapinga mafikiano hayo. Wajumbe katika mkutano huyo, walijikaza kisabuni ili kupata suluhu katika hoja ambayo hakika ilikuwa ya dharula. Maji taka Mkutano huu uliwaleta pamoja wajumbe zaidi ya 17,000 kutoka nchi 200 duniani, uliafiki   kurefushwa Mkataba wa Kyoto unaodhibiti uzalishaji gesi za nyumba ya kioo hadi mwaka 2020.   Isitoshe,nchi 27 za Umoja wa Ulaya, Australia na Uswisi na nchi nyingine nane zenye maendeleo ya viwanda zimekubali kushikamana na makubalino ya kuzuia uzalishaji wa gesi hizo hadi mwaka 2020. Hata hivyo,Marekani imekataa kutia saini Mkataba wa Kyoto. Pia   makubaliano hayo hayazihusishi nchi zinazochafua kwa kiasi kikubwa mazingira kama China na India. Katika hotuba yake , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon,aliunga mkono hatua hiyo na kuzisitiza kuwa n...

pamoja tuangamize saratani

Picha
Ni muhimu kudumisha usafi kinywani.Kusungua meno baada ya kula ilikuepikana na magonjwa kama vile  Saratani ya mdomo.saratani hii husambaa kinywani kwenye ulimi na koromeo.Ugonjwa huu huchukua muda mrefu kabla kutambuli.Wanaovuta sigara,kuvuta tumbako au kunywa pombe wamo hatarini mwa kupata saratani ya mdomo. Saratani ya mdomo ina inaweza kutibiwa unaweza kitibiwa ukiwahiwa mapema. Ishara ya saratani yam domo ni kama zifuatazo;   Uvimbe sehemu yoyote mdomoni, ambao hauponi kutokuwa na damu kwa urahisi. Kufa ganzi mdomoni. Kuhisi uchungu unapo tafuna, kumeza chakula ulimi unapotumika. Kubadilika kwa sauti. Kuumwa na sikio. Koo linalowasha bila kupona. pamoja tuangamize saratani