Jumamosi, 15 Desemba 2012

Mandela hospitali



 
Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea kupokea matibabu hospitali mjini Pretoria ambako anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.

Mzee Mandela alipelekwa na kulazwa hospitali, Jumamosi(wiki moja iliyopita).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea, Mandela naendelea kupata nafuu.

Mapema mwaka huu, Mandela alilazwa hospitali ili kutibiwa matatizo ya tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu.

Homa ya mapafu, husababishwa na viini tete vijulikanavyo kama (Streptococcus pneumoniae) na huathiri sehemu za kupumua kwenye mapafu.

Bwana Mandela amewahi kutibiwa kwa mara nyingine ugojwa wa kifua kikuu unaoathiri mapafu.

Magonjwa mengi ya mapafu hutibiwa kwa madawa , mgonjwa kupumzika au kupata vinywaji vingi.
  
Wazee na watu ambaom hawakinga ya mwili ndiyo huadhiriwa na maradhi haya.
Bwana Mandela ana miaka 94.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni