Jumanne, 18 Desemba 2012

WHO Malaria Kenya


Kenya yatoa ripoti zisizo kamili

Serikali ya Kenya imepiga hatua kukabiliana na ugonjwa wa malaria,ingawa hatua zake hazijaridhisha Shirika la Afya Duniani.






Kulingana na ripoti iliyotolewa rasmi na Shirika la Afya Duniani(WHO),tathmini ya maendeleo ya Kenya kupambana na malaria haiwezi kufanywa kwa sababu takwimu zake si kamili kudhibitisha juhudi zake za kuukabili ugonjwa wa malaria.

WHO imetaja Kenya kuwa miongoni mwa nchi saba katika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambazo viwango vya maambukizi vingali juu,huku huduma za afya zikiwa mbali na wananchi.


Zaidi ya hayo, serikali ya Kenya ilitoa ripoti kudhibitisha kutumia Dollar za Marekani 2,700,000 katika mipango yake ya kupambana na malaria katika mwaka 2010.Hata hivyo hakuna takwimu zinapatikana ama zilizotolewa katika kipindi za  2011.


Katika kipindi za 2010 Kenya ilipata Dollar za Marekani 39,100,000 kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa iliyofadhiliwa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi , Kifua Kikuu na Malaria(Global Fund).Ufadhili huo ulipunguzwa hadi Dollar za Marekani $ 12,200,000 mwaka 2011.



Rwanda,Zanzibar na Eritrea zimetajwa kama nchi ambazo zimepiga hatua  katika juhudi za kuukabili ugonjwa huu.Idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini Rwanda pia ilipungua kwa asili mia 75 mwaka wa 2000-2011.Haya yakiwa mafanikio makubwa.

 

Shirika la Afya Duniani imesema kuwa  harakati za kudhibiti ugonjwa huo ilipata msukumo mkubwa katika kipindi cha mwaka 2004 na 2009, lakini mwamko huo ulishuka katika kipindi cha mwaka 2010 na 2012.Jambo ambalo si lakuridhisha.

Shirika la Afya duniani (WHO), imezinduliwa  rasmi ripoti  hii ya mwaka 2012 inayoaangazia tatizo la Malaria katika mji Mkuu wa Liberia, Monrovia ,huku Rais Ellen Johnson Sirleaf, akilalama kuwa ripoti hii imeonyesha kushuka kwa jitihada za kukabiliana na kasi ya ugonjwa huo.

Zaidi ya watu  660,000 wakiwemo watoto wa umri chini ya miaka mitano warifariki kutokana na ugonjwa wa malaria mwaka jana.














 Malaria

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama Plasmodium ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya anopheles.
Dalili za malaria
  • Homa,maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mwili
  • Tumbo kuuma,kuharisha
  • Kichefuchefu,kutapika
  • Kupumua kwa shida
  • Kizunguzungu
  • Kutokwa jasho
  • Kutetemeka
  • Kifua kuuma
  • Kukosa hamu ya kula
  • Upungufu mkubwa wa damu mwilini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni