Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2013

midwife

Wakunga na uzazi Usimtukane   mkunga na uzazi ungalipo.Hii ni methali inayotuonya tusiwadharau au kuwatukana watu tunaowahitaji kwa jambo moja au nyingine, maishani Kwa muda mrefu,wakunga wamekuwa wakitoa huduma zao kwa kina mama wajawazito hivyo basi wanaheshimika sana katika jamii.   Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki muhimu sana kwani umoja wa mataifa ulitenda siku ya kuadhimisha Fistula   na pia mkutano wa wakunga duniani unaofanyika Kuala lumpur Hii ni dhahiri kuwa afya ya uzazi inapewa kipao mbele duniani. Wakati wa kujifungua kwa mwanamke, anakuwa kwenye hatari zaidi. Wengi huvuja damu hadi kufa, wengine hupangi na tundu katika sehemu zao za uzazi-fistula.Pia anaweza akampoteza mwanawe katika hali ile ya kujifungua. Ni kwa sababu hii akina mama wanahimizwa kuhudhuria vituo vya afya kwa uchunguzi na mafunzo ya kiafya. Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa,Wakunga wamechukua wajibu mkubwa katika jitihada za kupunguza h...