Alhamisi, 23 Mei 2013


''Congo Makao makuu ya ubakaji duniani''

vita dhidi ya Fisula


Huku dunia ikiadhimisha siku ya fistula duniani,ninachukua hii fursa kutakia akina mama  wa Goma afueni.
Kwa muda mrefu hali katika mashariki ya Congo imekuwa ya kuhuzunisha.
Akina mama wanauawa,kubakwa na pia kuolewa na waasi wa maeneo hayo.

Genevieve* mama mwenye watoto watatu wakati mmoja walisimulia jinsi alivyobakwa na wanaume watano na kupata fistula,lakini hakupata matibabu kwa siku sita, jambo lilipelekea hali yake ya kiafya kuzorota.
Mwanamke kuwa na hali hii anastahili upasuaji wa dharura ilikurekebisha hali yake.


 
Kutembea kwa muda mrefu ilikutafuta matibabu na pia gharama ya matibabu kumechangia wananwake wengi kuishi na fistula.

kutengwa na kudharauriwa ni baadhi ya unyanyapa wanawake wanaopitia kila siku Congo.

Imekuwa ni hali ya majonzi, kilio ma mahangaiko huku wasijue lakutenda.
Jana kundi la waasi la M23 wanakisiwa kushambulia wakazi wa Goma waadhiriwa wengi wakiwa akina mama.




Hali hii ilipelekea mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia ukatili katika mambo ya ngono kusema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio" makao makuu ya ubakaji duniani".

Hakika ukatili dhidi ya wanawake imekita mizizi Congo.Makundi ya waasi yanazurura mashariki mwa Congo na yote yanatuhumiwa kwa kuhusika na ukatili dhidi ya wanawake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni