Obstetric fistula
Katika baadhi ya mikoa hapa nchini Kenya, akina mama waja wazito hulazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta matibabu.Baadhi yao hulazimika kujifungua nyumbani ,jambo ambalo husababisha madhara ya kiafya.
Uchungu wa muda mrefu,kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu au kujifungua katika mazingira yasiyofaa ni chanzo cha ugonjwa unaojulikana kama fistula.
Kulingana
na daktari wa afya ya uzazi katika hospitali moja hapa jijini
Nairobi,Fistula ni tatizo linalotokana na jeraha wanalopata kina mama
wakati wa kujifungua baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na pia kuwa
na njia ndogo ya uzazi kiasi kwamba kichwa cha mtoto kinashindwa kupita
kwa usalama wakati wa kujifungua.
Hali hii humfanya mama kushindwa kujizuia wakati anapotaka kwenda haja ndogo na wakati mwingine hata kubwa bila mpangilio.
Ugonjwa huu ,umehatarisha maisha ya akina mama wengi.
Takwimu za Shirika Afya Duniani (WHO) sinadhihirisha ya kuwa zaidi ya wanawake milioni nne ulimwenguni kote wanaishi na fistula .
Daktari wanatilia mkazo haja ya wanawake wajawazito kutembelea kliniki za afya mara tu wanapotunga mimba ,ili kupata utalamu na mawaidha ya afya,hili kupunguza hatari.
Nchini
Kenya kuna baadhi ya mashirika ya afya yaani mashirika yashiyo ya
serikali ,yanayotoa matibabu ya bure kwa baadhi wa wanawake ambao
wamejikuta kwenye lindi hili na masonokeko.
Jambo la kutia moyo ni kuwa tatizo hili linaweza kutatuliwa.Baadhi ya wanawake niliowahoji wanasema kuwa baada ya upasuwaji na watalaamu wa afya ya uzazi,walirejea katika hali zao za kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni