Jumatatu, 27 Mei 2013



Wakunga na uzazi
Usimtukane  mkunga na uzazi ungalipo.Hii ni methali inayotuonya tusiwadharau au kuwatukana watu tunaowahitaji kwa jambo moja au nyingine, maishani

Kwa muda mrefu,wakunga wamekuwa wakitoa huduma zao kwa kina mama wajawazito hivyo basi wanaheshimika sana katika jamii.



 
Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki muhimu sana kwani umoja wa mataifa ulitenda siku ya kuadhimisha Fistula  na pia mkutano wa wakunga duniani unaofanyika Kuala lumpur
Hii ni dhahiri kuwa afya ya uzazi inapewa kipao mbele duniani.
Wakati wa kujifungua kwa mwanamke, anakuwa kwenye hatari zaidi.
Wengi huvuja damu hadi kufa, wengine hupangi na tundu katika sehemu zao za uzazi-fistula.Pia anaweza akampoteza mwanawe katika hali ile ya kujifungua.

Ni kwa sababu hii akina mama wanahimizwa kuhudhuria vituo vya afya kwa uchunguzi na mafunzo ya kiafya.
Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa,Wakunga wamechukua wajibu mkubwa katika jitihada za kupunguza hatari zinaowakumba wanawake wanapojifungua. Wakiwa na ujuzi wa juu, wakunga sasa wanaweza kukubiliana na  hatari zinaowakumba akina mama na wana wajibu mkubwa wa kuyaweka maisha  ya mama kuwa salama kote duniani.

Wakunga huwauguza akina mama kabla na baada ya kujifungua, wanalinda afya za watoto wanaozaliwa , wanatoa ushauri kuhusu upangaji uzazi, wanazuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wanafahamu wakati wa kuitisha huduma za dharura.
 
Inakadiriwa kuwa wakunga walio na mafunzo na wanaopata msaada wanaweza kuokoa  maisha ya zaidi ya wanawake 200,000 kila mwaka na mara kumi zaidi ya watoto kiasi hicho.
Washiriki katika kongamano na kuala lumpa wanasema kuna haja ya kuongeza idadi ya wakunga duniani ilikuepuka maafa yanayotokea wakati wakujifungua.

Pia hamazisho kwa akina mama ni muhimu;jambo ambalo mataifa yanayositawi na pia yaliostawi yanalitilia mkazo.
Ingawa pia wakunga wa jadi wanaheshimiwa kwa huduma zao, mara kwa mara hawana vifaa maalum endapo mama atashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.Hivyo basi wanahitaji kuelimishwa jinzi ya kukambiliana na hali za dharula.



Gharama za matibabu na umbali wa vituo vya afya ni changamoto ambalo pia ninastahili kushughulikiwa kwa haraka na serikali husika.

Endapo malengo yamilenia ya afya ya uzazi itaafikiwa basi ni sharti wahudumu wa afya washirikishwe .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni