leo ni siku ya kuadhimisha ugonjwa wa fistula duniani.
Je Fistula ni nini ?
Fistula ni ugonjwa hatari ambapo tundu hutokea kwenye mlango wa uzazi. Tundu hili linaweza kutokea kati ya uke na njia ya haja kubwa au kati ya kibofu na uke baada ya mama kushindwa kujifungua au kutumia muda mrefu kujifungua.
Pia kunajisiwa kunaweza kusababisha hali hii.
Matokeo yake ni kwamba wanawake wenye fistula hujikuta katika matatizo makubwa ya kutokwa ovyo na mkojo au na kinyesi.Mara kwa mara wao hutengwa na jamii na kudharauriwa.Mwishowe wengi hujitia kitanzi kwa sababu ya machungu.
Kenya ni nchi ambazo zimepiga hatua kuhakikisha angalau akina mama na wakenya wa jumla wamehamasishwa kuhusu madhara yake ya namna ya kukakabili hali hii.
kulingana na takwimu za UNFPA zaidi ya visa 3,000 hulipotiwa kila mwaka huku.
Kuna hospitali chache hapa nchini ambazo zinafanya upasuaji wa kurekebisha hali hii, kama Hospitali kuu ya Kenyatta na Moi referal,Eldoret.
Hata hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wakenya wamepata mafunzo kuhusu afya ya uzazi ili wajue kuna tiba ya fistula.
Hali ya wasichana wadogo kukumbwa sana na fistula ya uzazi inahusishwa kwa karibu zaidi na kutokomaa vizuri kwa miili yao na nyonga zao. Mara nyingi fistula ya uzazi huwakumba watu wanaoishi maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba mkubwa sana wa watoa huduma wenye ujuzi.
zaidi ya hayo,baadhi ya watu niliowahoji hawajui kuna tiba ya fistula hasa vijini.
Wengine hawajui aina za mpango wa uzazi walio chini ya miaka kumi na nane na ushirini. ukosefu wa ushauri kwa hakika kunachangia wasichana wengi kujikuta katika hali
Mwaka wa 1992 na 2001 upazuaji kerekebisha hali hii uliongezeka kutoka 36 hasi 479 kwa mwaka.Hatua ya kujia moyo ingawa mengi yahitajika.
Tuna watakia akina mama wanaojifungua baraka zake maulana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni