Madaga afariki baada ya kukosa matibabu ya dharura kwa muda wa masaa kumi na nane.
Mgonjwa ambayo alikosa matibabu ya dharura kwenye hospitali kuu ya Kenyatta ameaga .
Alex Madaga alisubiri kwa muda mrefu kupata nafasi na matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufikishwa pale hospitalini baada ya kugongwa na gari kwenye barabara ya Waiyaki.
Kutokana na hali yake ya majeraha hospitali ya Kikuyu iliamuru apelekwe Kenyatta kwa haraka ilikuokoa maisha yake. Lakini mambo yakaenda mlama alipozungushwa hosptali kadha mjini Nairobi baadhi yao wakisema hawakuwa na vitanda vya wagojwa mahututi au walitaka pesa kiasi Fulani kabla ya matibabu.
zaidi.Unyama ulioje?Baadhiya hospitali cha kibinafsi na pia za umma zinamazoea ya kuwakataza matibabu wangojwa huku wakitaka malipo kabla ya matibabu kutolewa.
Hali hii imepelekea maafa kwa wagonjwa ambao wagepona endapo matibabu ya dharura yalitolewa.Kuyapa kipao mbele maswala ya pesa ni ulafi na kukosa utu.
Husuni na simanzi zimetanda kufuatia habari za kifo ambacho kingeepukika endapo hatua za dharura zingechukuliwa.
Mola awape amani familia na mwenda zake alale pema peponi.
Ijumaa, 9 Oktoba 2015
Kenyatta National Hospital ICU machines
Hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya imegonga vichwa vya vyombo ya habari hasa mwaka huu kwa uduni,upungufu au ukosefu wa vifaa maalum vya matibabu.
hata baada ya muda usio mrefu sasa imebainika kuwa kuna mashine thelathini pekee za wagonjwa mahututi na hii inasababisha msongamano hasa kwa wagonjwa wanaopelekwa Kenyatta kwa magonjwa ya dharura.
Majeruhi hasa wa ajali za barabarani husuburi kwa muda mrefu ndani ya abulensi huku wengine wakifariki kabla ya kupata nafasi kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni changamoto kwa serikali kuhakikisha hela za kutosha kinatengwa kwa wizara ya afya ilikukabili hali hii duni.
Ni jambo la kuhuzunisha kuona mgonjwa akifariki kwa sababu ambazo hakika zingeepukika endapo serikali iliwajibika.
Ufizadi pia unachangi hali kama hii kwenye hospitali za umma.
Kwa mfano utanunuaje vifaa ambavyo si muhimu kwa mamilioni ya pesa huku kutenga fedha zisizotosha kununua vifaa muhumu hospitalini.
Hospitaki kuu ya Kenyatta ,inahudumia mamilioni ya wakenya wanaotoka sehemu tofauti chini na pia wagojwa kutoka nchi jirani.
Janet Kanini Ikua lung cancer
MTANGAZAJI AUGUA SARATANI
Mtangazaji Janet Kanini Ikua
amegunduliwa kuna anaigua saratani ya mapafu.
Kanini alisema kupitia mtandao kuwa
ako nchini India ambako anaendelea kupokea matibabu.
Hapo awali Kanini alikuwa pia
alipatikana na ugonjwa wa damu kuganda kwenye misipa inayopeleka damu kwenye
roho.
Kiinim chake hasa kuzuru India ilikuwa ni kupokea matibabu ya ugonjwa huo ujulikanao kwa kimombo kama Deep Vein Thrombosis.
Dalili ya ugonjwa huu ni kufura miguu na pia kuwa na uchungu miguuni unaomfanya mgonjwa kuwa na matatizo ya kutembea.
Daktari wake aliyemtaja kama wakutajika nchini India amemhakikishia kuwa akiendelea na matibabu kwa muda wa miezi sita au zaidi atapona,ingawa unaweza ukarudi.
Kwa sasa anapokea matibabu kuhakikisha damu iliyoganda haifiki kwenye roho au moyo ambazo ni viungo muhimu sana mwilini.
deep vein thrombosis,
deep vein thrombosis,
deep vein thrombosis,
Hata baada ya hali yake hiyo Kanini
alisema anahakika kuwa Mola atamponya na atarejea nyumbani Kenya baada ya
matibabu.
ALISEMA nia ya kusema kuhusu hali yake
ilikuwa kuwapa motisha wengi wanaopitia hali kama hiyo ili wasife moyo na
waendelee na kutafuta matibabu bila wasiwasi.
Kulingana na takwimu za shirika la
afya ulimwenguni WHO idadi ya wanaougua ugonjwa wa saratani unaendelea
kuongezeka.
Ingawa ugomjwa huu ni baadhi ya
maradhi hatari ,inatibiwa na mgonjwa akapona,mradi atafute tiba mapema.
Kwa upande wa Kanini matibabu
yanachukuwa muda.Pia gharama ya matibabu nchini India gharama ni nafuu ikilinganishwa
na nchini Kenya.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)