Hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya imegonga vichwa vya vyombo ya habari hasa mwaka huu kwa uduni,upungufu au ukosefu wa vifaa maalum vya matibabu.
hata baada ya muda usio mrefu sasa imebainika kuwa kuna mashine thelathini pekee za wagonjwa mahututi na hii inasababisha msongamano hasa kwa wagonjwa wanaopelekwa Kenyatta kwa magonjwa ya dharura.
Majeruhi hasa wa ajali za barabarani husuburi kwa muda mrefu ndani ya abulensi huku wengine wakifariki kabla ya kupata nafasi kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni changamoto kwa serikali kuhakikisha hela za kutosha kinatengwa kwa wizara ya afya ilikukabili hali hii duni.
Ni jambo la kuhuzunisha kuona mgonjwa akifariki kwa sababu ambazo hakika zingeepukika endapo serikali iliwajibika.
Ufizadi pia unachangi hali kama hii kwenye hospitali za umma.
Kwa mfano utanunuaje vifaa ambavyo si muhimu kwa mamilioni ya pesa huku kutenga fedha zisizotosha kununua vifaa muhumu hospitalini.
Hospitaki kuu ya Kenyatta ,inahudumia mamilioni ya wakenya wanaotoka sehemu tofauti chini na pia wagojwa kutoka nchi jirani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni