Ijumaa, 9 Oktoba 2015

Madaga aaga dunia

Madaga afariki baada ya kukosa matibabu ya dharura kwa muda wa masaa kumi na nane.

Mgonjwa ambayo alikosa matibabu ya dharura kwenye hospitali kuu ya Kenyatta ameaga .
Image result for madaga dies after accident

 Alex Madaga alisubiri kwa muda mrefu kupata nafasi na matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufikishwa pale hospitalini baada ya kugongwa na gari kwenye barabara ya Waiyaki.

Kutokana na hali yake ya majeraha hospitali ya Kikuyu iliamuru apelekwe Kenyatta kwa haraka ilikuokoa maisha yake. Lakini mambo yakaenda mlama alipozungushwa hosptali kadha mjini Nairobi baadhi yao wakisema hawakuwa na vitanda vya wagojwa mahututi au walitaka pesa kiasi Fulani kabla ya matibabu.

 zaidi.Unyama ulioje?Baadhiya hospitali cha kibinafsi na pia za umma zinamazoea ya kuwakataza matibabu wangojwa huku wakitaka malipo kabla ya matibabu kutolewa.
Hali hii imepelekea maafa kwa wagonjwa ambao wagepona endapo matibabu ya dharura yalitolewa.Kuyapa kipao mbele maswala ya pesa ni ulafi na kukosa utu.

Husuni na simanzi zimetanda kufuatia habari za kifo ambacho kingeepukika endapo hatua za dharura zingechukuliwa.
Mola awape amani familia na mwenda zake alale pema peponi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni