Jumatano, 7 Oktoba 2015

Wangari maathai road

 Msitu wa karura ulimpa umaarufu Marehemu Prof. Wangari Maathai
Juhudi za hayati Wangari Mathaai za kuhifadhi mazingira zatambuliwa na jimbo la jiji la Nairobi na kumtunuku  kwa kubadilisha njia ya Limuru na kuipa jina mpya ya Wangari Mathaai.
Image result for wangari maathai 
Maathai alikuwa mwanamazingira maarufu aliyejitolea mhanga kuhakikisha wanyakuzi wa ardhi walikabiliwa vilivyo.
 Barabara ya Limuru inapitia kwenye msitu wa karura na pia ni njia ambayo inaelekea kwenye makao makuu ya uhifadhi wa mazingira ya Umoja wa Mataifa,Nairobi.
Zaidi ya hayo,Kuna bustani nchini Peru ambayo pia imepewa jina la Wangari Maathani.Na pia Marekani na Japani.
 Mama Mathaai aliaga dunia miaka minne iliyopita baada ya kuugua  saratani ya mfuko wa uzazi(Ovarian Cancer)

Marehemu Maathai alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004 na kuwa mwanamke wa kwanza mwafrika, mkenya wa kwanza na mwanamazingira wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo.

Umaarufu wa Mathaai ulitokana na ari yake ya Mazingira.Alikuwa kwenye mstari wa mbele kuelimisha wakenya na ulimwengu kwa ujumla umuhimu wa  kuhifadhi na kutunza mazingira.

Pia alipigia debe jitihada za kutimiza lengo la milenia la kutunza na kulinda mazingira.


Karne tatu zilizopita, Maathai aliasisi shirika la mazingira nchini Kenya, Kenya Green Belt Movement.
chemichemi ya maji

Alikuwa mama shujaa na pia  mkakamavu ambaye hakutishwa na yeyote.Alifanya kazi yake aliyoienzi kwa dhati.

Wanyakuzi alihakikisha mipango yao imetibuliwa.Alifanya kampeni ya kupinga ujenzi wa majengo mawili katika bustani ya Uhuru.

Zaidi ya hayo, aliandamana na wanaharakati wa mazingira hadi Mlima Kenya kungoa bangi.Shughuli ya upandaji bangi ndani ya msitu wa mlima Kenya ilikuwa imekidhiri hadi alipoingilia kati.

Maathai alikuwa mashuhuri kote duniani na alipanda miti popote alipozuru.




 Mwaka wa 2002, aliibuka mshindi wa kiti cha ubunge cha Tetu.Vilevile,aliteuliwa na rais Mwai Kibaki kuwa naibu waziri  wa mazingira, wadhifa alioushikilia hadi mwaka mwa 2005.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni