Ijumaa, 31 Mei 2019

Rais Uhuru Kenyatta Canada Conference


Image result for president kenya and trudeauKongamano la jinsia Vancouver,Canada
Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ataondoka nchini wiki ijayo kuelekea nchini Canada kuhudhuria kongamano la maswala ya jinsia na afya ya akina mama na wasichana ilioadaliwa na shirika la Women Deliver.
Rais Kenyatta ni miongoni mwa wakuu wa mataifa na serikali waliopokea mwaliko wa waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.Mkutano huo utaadaliwa jumatatu hadi jumatano wiki hii ,utaangazia maswala ya ya jinsi, afya na haki za wanawake.
Wadaukutoka sekta ya afya,vijana,wasomi,wanaharakati na waandishi wa habari kutoka nchi zaidi ya elfu sita(6,000) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu.
Nchini ya kenya ni miongoni mwa nchini ambazo zinajitahidi kupiga hatua katika maswala na jinsia na haki za akina mama.
Serikali,kupitia bima ya afya ya kitaifa inatoa huduma ya linda mama ;huduma hii inasaidia wa mama kupata huduma ya matibabu ya bure wanapoeenda kujifungua popote nchini kenya.
Mama waTaifa ,Margaret Kenyatta pia amekuwa katika mstari wa mbele kuchangia katika afya ya akina mama hasa wenye uja uzito.
Amekuwa akifanya mbio za kuchangisha pesa ili kuhakikisha akina mama waja wazito na waliojifungua na watoto wao wanapata matibabu bila malipo.Huduma hii inawasaidia walio mashinani kufikiwa na huduma za afya bila vikwazo.
Rais atahutubia mkutano huo na pia atafanya mikutano ya mubadala na mwenyeji wake Justin Trudeau.


Women deliver,Vancouver,Canada 2019



Women Deliver 2019 Conference 

Shirika linalo ongoza katika juhudi za kutetea haki na afya ya akina mama , Woman Deliver imetayarisha kongamano la usawa wa jinsia,haki na ustawi wa wasichana na wanawke utakaofanyika huko Vancouver nchini Canada mwanzoni mwa mwezi wa Juni mwaka huu.
Mkutano huu unalenga maswala ya jinsia na afya ya akina mama na wasichana katika karne ya 21.

Wadau kutoka sekta ya afya,vijana,wasomi,wanaharakati na waandishi wa habari kutoka nchi zaidi ya elfu sita(6,000) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu.Waakilishi kutoka  Shirika la afya ulimwenguni,WHO watajiunga na wadau hawa katika mkutano huu unaotajwa kama mkubwa kufanyika Canada.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus, anasema usawa  wa kijinsia lazima uwe msingi wa afya kwa wote .
Rais wa Women deliver Katja Iversen anasema shirika lake limejitolea kuwapa matumaini akina mama kwa vitendo na sio kwa maneno matupu.
Image result for dr tedros adhanom ghebreyesusAnasema kuwa huu ni mkutano wa tano kufanyika duniani na canada imepiga hatua ya kuigwa na nchi zingine duniani.Iversen anamatumaini mkutano huu utakuwa na matokeo na faida nyingi kwa wanawake n watu wote kwa ujumla.
Mada kuu ya mkutano huu ni kuhakikisha maswala na akina mama na wasichana napewa kipao mbele ili kufanya duniani bora zaidi.
Haki za mama za kiafya,kielimu na maswala nanayohusiana na uzazi wa mama unatiliwa maanani hapa huku ikifahamika kuwa akina mama wanachanga moto za kifya .Mwanamke mwenye afya bora anatekeleza majukumu yake bila tatizo.Hii inachangia kwenye uchumi wa nchi kwani akina mama wana changia kukua kwa chumi za nchi kote duniani.
Idadi ya akina mama pia inaongoza ikilinganishwa na ya wanaume kote duniani.
Hivyo basi mchango wao hauna budi kuheshimiwa.

Changamoto zipo zinazowakabili akina mama kila siku kama vile ukosefu wa huduma za afya karibu na makazi yao.Hasa akina mama wajawazito ambao hulazimika kutumbea muda mrefu kutafuta huduma za afya.Nchi zinazoendelea zikiadhirika zaidi.Bei ya matibabu ni swala ambalo pia limekuwa ngumu.
Sio wengi hususani akina mama wa mashambani wanao uwezo wakulipa gharama ya matibabu.

Katika mkutano wa Canada maswala yote haya yatatafutiwa mikakati mwafaka na suluhu kuhakikisha akina mama na wasichana wamepata haki zao za kiafya na kijumla.
Waziri mkuu wa Canada ,Justin Trudea  amewakaribisha wanaohudhuria kongamano.
Image result for women deliver presidentImage result for women deliver 2019Amewataka kutumia muda wao kujadili maswala ya jinsi ;na kutafuta mikakati ya kudumu.

 Elimu ya uzazi wa mama pia ni ya muhimu,kupitia hii elimu mwanamke anaelimika na kujua haki zake za uzazii ,jinsia na jinsi ya kuzitekeleza au kufuata haki hizo anapokuwa kwenye tatizo fulani la kiafya au kiajamii.
Bila kutatua changamoto hizi itakuwa ni vugumu kufikia malengo au agenda ya afya na maendeleo endelevu ifikapo mwaka wa 2030.
Kongamano hii inafanyika wakati muhimu sana katika maisha ya wanawake kiafya ,kielimu na kiuchumi.

Hasa nchini Canada wamepiga hatua marudufu kuhakikisha haki hizi zimetekelezwa.
Kuna pia baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimepiga hatua na kuweka maswala ya jinsia  mstari wa mbele ili kuendeleza jamii na taifa kwa jumla.
Mkutano huu utafuatilia kwa kina maswala yaliojadiliwa hapo mwanzo katika kongamano lililofanyika Copenhagen,Denmark mwaka wa 2016.

Namna ya kutatua ,Ndoa za mapema ,sodo za wanawake na ukeketaji ni maswala yaliojadiliwa hapa.

Rais wa Ethiopia,Sahle Work Zewde na Mke wa Waziri Mkuu wa Canada,Sophie Trudeau ni miongoni mwa watakaohutubia kikao hiki.

Kongamano la shirika la Women Deliver hufanyika kila baada ya miaka mitatu. 




Alhamisi, 30 Mei 2019

Tobacco day 2019 -Tumbaku



Maadhimisho ya siku ya kimataifa duniani ya kutovuta tumbaku yatafanyika kesho, Ijumaa.
Shughuli hii hufanyika kila mwaka ,lengo likiwa kuwatahadharisha watu adhari za ufutaji au utumiaji wa tumbaku kwa afya ya watu.
Mwaka huu kauli mbinu ikiangazia matumizi ya tumbaku na adhari zake kwa mapafu ya mwanadamu,”Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako
Shirika la afya ulimwenguni, WHO inakadilia kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo vihusianavyo na utumiaji wa tumbaku ni kama vile magonjwa ya saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa na Kifua Kikuu.WHO inataka serikali na wadau wana jukumu la kuhakikisha hatua za kulinda watu dhidi ya tumbako zimeongezwa.
Mkurugenzi WHO,Daktari Tedros Ghebreyesus  amenukuliwa akisema kuwa,kila mwaka watu wapatao millioni  nane hufariki kutokana na matumizi ya tumbako.
Zaidi ya hayo,mamilioni ya watu duniani wanaishi na magonjwa  yanayosababishwa  na madhara ya utumiaji tumbaku.
Anasema Dkt Ghebreyesus kuwa kwa mtu kuishi maisha marefu na kuwa na mapafu yenye afya ni sharti ajiepushe na tabia za kutumia tumbaku.
Watu wengi huadhirika na matumizi ya tumbaku hasa marafiki ,jirani au jamii inayokaa pamoja na watu au mtu anayetumia tumbaku.
Kulingana na wataalamu wa afya anayeadhirika Zaidi ni yule asiyetumia lakini ako mkabara au karibu na mtumiaji.
Watoto pia wameadhiriwa na hali hii.WHO inasema Zaidi ya watoto elfu sitini(60,000) wenye umri wa chini ya miaka 5 hufariki dunia kutokana na kuvuta moshi wa wavutao sigara.
Pia wanaoishi hadi kufikia utu uzima wao huwa kwenye hatari ya kupata magonjwa hatari ya mapafu na njia ya hewa.
moshi wa sigara na adhari zake
 Nukuu za WHO sinaonyesha kuwa mvuto mmoja tu wa moshi wa sigara una mamia ya kemikali za sumu ambazo huharibu mapafu pole pole hadi inafika kiwango cha hatari kinacho haribu mapafu.
Sumu iliyomo kwenye tumbaku hudhoofisha mifumo ya kusafisha makohozi na uchafu huku ikiadhiri mapafu.
Image result for tobacco act in kenya
Hali hii imechangia mtu kukosa pumzi au kuwa na ugumu wa kupumua huku njia za hewa zikipata uvimbe na kujenga kohozi na mwishowe mapavu yanaharibika kabisa.Mwishowe ni kudhoofika kwa afya na baadaye kifo mbacho kingeepukika endapo utumiaji wa sigara ungetupiliwa mbali.
 Nchini kenya hatua zimechukuliwa kuhakikisha kuwa watu wameelimishwa kuhusu madhara ya tumbaku.
Kwenye ofisi za umma na za kibinafsi kuna vibao vinavyotua ilani kuwa ufutaji sigara au tumbaku kunadhuru afya ya mtu.Lakini hata baada ya mafufuku ya uvutaji sigara kutolewa wengi huwa hawavitilii maanani,wanapuuza bila kujali afya yao.
Suluhu
Shirika la fya duniani WHO inasisitiza haja ya serikali kutokomeza janga la tumbaku kwa kutekeleza kwa kina mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumzi ya tumbaku, na kuimarisha hatua dhidi ya matumizi ya tumbaku.
HIi imeafikiwa kwa kiwango Fulani nchini kenya kwani kodi za sigara zimewekwa juu zaisi
Pia maeneo yametengwa kwa wavuta sigara ili wasitangamane na wasiovuta
Kuelimisha jamii madhara ya sigara na mbinu za kujiepusha na matumizi;serikali pia imepiga hatua kuona kuwa elimu inatolewa mara kwa mara kwa jamii.
 Endapo suluhu hizi zitakuwa na mafanikio,basi ifikapo mwaka wa 2030 idadi ya wanaoadhiriwa na hali hii itapunguka kwa kiwango cha theluthi moja.