Ijumaa, 31 Mei 2019

Rais Uhuru Kenyatta Canada Conference


Image result for president kenya and trudeauKongamano la jinsia Vancouver,Canada
Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ataondoka nchini wiki ijayo kuelekea nchini Canada kuhudhuria kongamano la maswala ya jinsia na afya ya akina mama na wasichana ilioadaliwa na shirika la Women Deliver.
Rais Kenyatta ni miongoni mwa wakuu wa mataifa na serikali waliopokea mwaliko wa waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau.Mkutano huo utaadaliwa jumatatu hadi jumatano wiki hii ,utaangazia maswala ya ya jinsi, afya na haki za wanawake.
Wadaukutoka sekta ya afya,vijana,wasomi,wanaharakati na waandishi wa habari kutoka nchi zaidi ya elfu sita(6,000) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu.
Nchini ya kenya ni miongoni mwa nchini ambazo zinajitahidi kupiga hatua katika maswala na jinsia na haki za akina mama.
Serikali,kupitia bima ya afya ya kitaifa inatoa huduma ya linda mama ;huduma hii inasaidia wa mama kupata huduma ya matibabu ya bure wanapoeenda kujifungua popote nchini kenya.
Mama waTaifa ,Margaret Kenyatta pia amekuwa katika mstari wa mbele kuchangia katika afya ya akina mama hasa wenye uja uzito.
Amekuwa akifanya mbio za kuchangisha pesa ili kuhakikisha akina mama waja wazito na waliojifungua na watoto wao wanapata matibabu bila malipo.Huduma hii inawasaidia walio mashinani kufikiwa na huduma za afya bila vikwazo.
Rais atahutubia mkutano huo na pia atafanya mikutano ya mubadala na mwenyeji wake Justin Trudeau.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni