Jumatano, 29 Mei 2019

menstrual hygiene day-Hedhi

Huku dunia ikiadhimisha siku ya hedhi, maswala ya hedhi na usafi wake yangali ni changamoto hususan barani Afrika.

Jane Muthoni ni msichana wa umri wa miaka kumi na tayari anapata hedhi kila mwezi.
Yeye ni mwanafunzi wa shule ya msingi darasa la nane katika maeneo ya Kabiti Muranga.
Kwa muda mrefu Muthoni amekubwa na changamoto tele wakati wa hedhi.

Mara hana sodo au ana maumivu ambayo umfanya akose kwenda shuleni.
Pia ana ona haya kwenda shuleni kwa kuogopa hedhi kuvuja na kuchekelewa na wenzake.
Hii imepelekea yeye kupotesa muda wengi kila mwezi na mwaka kwa jumla.
Masomo yake yameadhirika pakubwa na amewahi kurudia darasa kotokana na matekeo duni ya mtihani wa kila mwaka.

Anasema anatumia matabara ambayo damu huvuja baada ya muda mfupi,jambo ambalo limemadhiri pia kimawazo.
Angetaka serikali iweke mikakati ya kuhakikisha kila mtoto wa kike ambaye anapata hedhi ,ana taulo au sodo kila mwezi na pia maji iwepo shuleni ilikudhumisha usafi.
Anasema vyoo wanavyo tumia pia ni changamoto kwani ni chafu na ambazo hazistahili kutumiwa.

Anapendekeza;kuwe na vyoo na vyombo maalum za kuhifadhia sodo baada ya matumizi
Muthoni ni baadhi ya wasichana wanaolengwa kupata elimu kuhusu hedhi na umuhimu wa usafi wakati wa hedhi na mashirika isiyo ya kiserikali na watu binafsi wanaojitolea kuhakikisha wasichana hawakosi masomo juu ya hedhi.
Jacinta Wanjiru pia ni mwanafuzi wa kike anayeishi na kusomea Korogocho katika mtaa duni.
Maisha katika mtaa huu ni magumu Zaidi;ukosefu wa maji safi,vyoo na hata kupata pesa za kujikimu kimaisha ni changamoto.
Yeye kama wenzake alipata hedhi kwa mara ya kwanza mwezi uliopita na hakuwa na habari ya kutosha jinsi ya kujistiri wakati huo.
Anasema vijana shuleni walimchezea alipojipata amevuja damu wakati wa hedhi.Anasema alipata pia changamoto ya kupata sodo kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo.Ilibidi abaki nyumbani hadi siku ya tatu huku akidanganya mwalimu wake kuwa alikuwa anauguwa.

Ilibidi afanye urafiki na kijana wa jirani ambaye alimsaidia kupata hela ya kununua sodo.
Wasichana wengi hapa hufanya mapenzi na wanaume ili wapate pesa za kununua sodo.”usipofanya hivyo utaumia wewe mwenyewe ,anafichua Wanjiru.
Anasema wazazi pia wanajukumu lakuelimisha wasichana changamoto za hedhi na kuwasaidia katika vipindi hivyo.

Wazazi wengi huwaachia majukumu ya mafunzo ya kijamii waalimu lakini si vema.wanapaswa watusaidie pia ,Wanjiru anasema.
Nchi zinazoendelea zina sababu ya kuelimisha watu umuhimu wa usafi na utumiaji wa vifaa vya hedhi vilivyokanguliwa viwango vyake na kukubalika kama kamili kutumiwa.
Mataifa ya Afrika yametilia mkaso elimu ya hedhi na pia gharama yake ,yaani bei ya sodo.
 Bali na hayo ni wachache hasa sehemu za nashambani walio na uwezo wa kugharamia sodo kulingana na ukosefu wa hela. 

Baadhi ya wasichana  kama Muthoni na pia akina mama hutumia matope ,magada ya ndizi au hata matabara wakati wa hedi . vifaa wanavyotumia vipindi vya hedhi huwa havistahili kutumiwa na vina madhara yake
Hali hii imepelekea serikali na wadau kutafuta mbinu ya kupata sodo kwa bei nafuu na kupeleka shuleni bila malipo.
Wasichana wanapewa sodo kila mwezi bila malipo na kufunzwa jinsi ya kudumisha usafi wakati wa hedhi.

Pia kuna kampuni zinazotengeneza sodo za bei ya nafuu.Lakini sio kila shule au jimbo linalobahatika kupata sodo shuleni.
Itakuwa ni vema endapo serikali za mashinani zitatilia maanani swala hili kuhakikisha kila msichana hasa wale walioko shuleni wamebahatika na mchango was ono na elimu ya hedhi kupelekwa kote nchini ili kutatua tisho na aibu inayotokana na hedhi.

Vikopo vya hedhi na jinsi ya kutumia
Zaidi ya hayo, kuna vikopo vya hedhi ambavyo vimetolewa na vinaweza kutumika kwa muda mrefu bora.Ingawa vikopo hivi vina bei ya juu vinadumu kwa muda mrefu na havivuji hivyo basi kuondoa hofu ya aibu kwa wanaovitumia.
Linalo hitajika ni kuosha punde tu baada ya matumizi.

Takwimu zinakadilia kuwa asilimia 65 ya wnawake wanatumia sodo zakujitengenezea wenyewe huku asilimia 42 ya wasichana walioko shuleni wakisema hawajawahi tumia sodo.

Asili mia 25 ya akina mama hutumia bidhaa za kienyeji wengi walikwa mashambani.
Zamani ilikuwa mwiko kuzungumzia maswala ya hedhi lakini mambo yamebadilika .Tuungane kuwasaidie wasichana kuboresha elimu na maisha yao kwa kuongea kuhusu hedhi bila uoga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni