Mkutano huu unalenga maswala ya jinsia na afya ya akina mama na wasichana katika
karne ya 21.
Wadau kutoka sekta ya afya,vijana,wasomi,wanaharakati na waandishi wa
habari kutoka nchi zaidi ya elfu sita(6,000) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano
huu.Waakilishi kutoka Shirika la afya
ulimwenguni,WHO watajiunga na wadau hawa katika mkutano huu unaotajwa kama
mkubwa kufanyika Canada.
Rais wa Women deliver Katja Iversen anasema shirika lake limejitolea kuwapa
matumaini akina mama kwa vitendo na sio kwa maneno matupu.
Mada kuu ya mkutano huu ni kuhakikisha maswala na akina mama na wasichana
napewa kipao mbele ili kufanya duniani bora zaidi.
Haki za mama za kiafya,kielimu na maswala nanayohusiana na uzazi wa mama
unatiliwa maanani hapa huku ikifahamika kuwa akina mama wanachanga moto za
kifya .Mwanamke mwenye afya bora anatekeleza majukumu yake bila tatizo.Hii
inachangia kwenye uchumi wa nchi kwani akina mama wana changia kukua kwa chumi
za nchi kote duniani.
Idadi ya akina mama pia inaongoza ikilinganishwa na ya wanaume kote
duniani.
Hivyo basi mchango wao hauna budi kuheshimiwa.
Changamoto zipo zinazowakabili akina mama kila siku kama vile ukosefu wa
huduma za afya karibu na makazi yao.Hasa akina mama wajawazito ambao hulazimika
kutumbea muda mrefu kutafuta huduma za afya.Nchi zinazoendelea zikiadhirika
zaidi.Bei ya matibabu ni swala ambalo pia limekuwa ngumu.
Sio wengi hususani akina mama wa mashambani wanao uwezo wakulipa gharama ya
matibabu.
Waziri mkuu wa Canada ,Justin Trudea amewakaribisha wanaohudhuria kongamano.
Elimu ya uzazi wa mama pia ni ya
muhimu,kupitia hii elimu mwanamke anaelimika na kujua haki zake za uzazii ,jinsia
na jinsi ya kuzitekeleza au kufuata haki hizo anapokuwa kwenye tatizo fulani la
kiafya au kiajamii.
Bila kutatua changamoto hizi itakuwa ni vugumu kufikia malengo au agenda ya
afya na maendeleo endelevu ifikapo mwaka wa 2030.
Kongamano hii inafanyika wakati muhimu sana katika maisha ya wanawake
kiafya ,kielimu na kiuchumi.
Hasa nchini Canada wamepiga hatua marudufu kuhakikisha haki hizi
zimetekelezwa.
Kuna pia baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimepiga hatua na kuweka maswala
ya jinsia mstari wa mbele ili kuendeleza
jamii na taifa kwa jumla.
Mkutano huu utafuatilia kwa kina maswala yaliojadiliwa
hapo mwanzo katika kongamano lililofanyika Copenhagen,Denmark mwaka wa 2016.
Kongamano la shirika la Women Deliver hufanyika kila
baada ya miaka mitatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni