Maadhimisho ya siku ya kimataifa duniani ya
kutovuta tumbaku yatafanyika kesho, Ijumaa.
Shughuli hii hufanyika kila mwaka ,lengo likiwa
kuwatahadharisha watu adhari za ufutaji au utumiaji wa tumbaku kwa afya ya
watu.
Mwaka huu kauli mbinu ikiangazia matumizi ya
tumbaku na adhari zake kwa mapafu ya mwanadamu,”Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako”
Shirika la afya ulimwenguni, WHO inakadilia
kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo vihusianavyo na utumiaji wa tumbaku ni kama
vile magonjwa ya saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa na Kifua Kikuu.WHO
inataka serikali na wadau wana jukumu la kuhakikisha hatua za kulinda watu
dhidi ya tumbako zimeongezwa.
Mkurugenzi WHO,Daktari Tedros Ghebreyesus amenukuliwa akisema kuwa,kila mwaka watu
wapatao millioni nane hufariki kutokana
na matumizi ya tumbako.
Zaidi ya hayo,mamilioni ya watu duniani
wanaishi na magonjwa yanayosababishwa na madhara ya utumiaji tumbaku.
Anasema Dkt Ghebreyesus kuwa kwa
mtu kuishi maisha marefu na kuwa na mapafu yenye afya ni sharti ajiepushe na
tabia za kutumia tumbaku.
Watu wengi huadhirika na matumizi
ya tumbaku hasa marafiki ,jirani au jamii inayokaa pamoja na watu au mtu
anayetumia tumbaku.
Kulingana na wataalamu wa afya
anayeadhirika Zaidi ni yule asiyetumia lakini ako mkabara au karibu na
mtumiaji.
Watoto pia wameadhiriwa na
hali hii.WHO
inasema Zaidi
ya watoto elfu sitini(60,000) wenye umri wa chini ya miaka 5 hufariki dunia
kutokana na kuvuta moshi wa wavutao sigara.
Pia wanaoishi hadi kufikia
utu uzima wao huwa kwenye hatari ya kupata magonjwa hatari ya mapafu na njia ya
hewa.
moshi wa sigara na adhari zake
Nukuu za WHO sinaonyesha kuwa mvuto mmoja tu wa
moshi wa sigara una mamia ya kemikali za sumu ambazo huharibu mapafu pole pole
hadi inafika kiwango cha hatari kinacho haribu mapafu.
Sumu iliyomo
kwenye tumbaku hudhoofisha mifumo ya kusafisha makohozi na uchafu huku
ikiadhiri mapafu.
Hali hii
imechangia mtu kukosa pumzi au kuwa na ugumu wa kupumua huku njia za hewa
zikipata uvimbe na kujenga kohozi na mwishowe mapavu yanaharibika kabisa.Mwishowe
ni kudhoofika kwa afya na baadaye kifo mbacho kingeepukika endapo utumiaji wa
sigara ungetupiliwa mbali.
Nchini kenya hatua zimechukuliwa kuhakikisha
kuwa watu wameelimishwa kuhusu madhara ya tumbaku.
Kwenye
ofisi za umma na za kibinafsi kuna vibao vinavyotua ilani kuwa ufutaji sigara
au tumbaku kunadhuru afya ya mtu.Lakini hata baada ya mafufuku ya uvutaji
sigara kutolewa wengi huwa hawavitilii maanani,wanapuuza bila kujali afya yao.
Suluhu
Shirika la fya duniani
WHO inasisitiza haja ya serikali kutokomeza janga la tumbaku kwa kutekeleza kwa
kina mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumzi ya tumbaku, na kuimarisha hatua
dhidi ya matumizi ya tumbaku.
HIi imeafikiwa kwa
kiwango Fulani nchini kenya kwani kodi za sigara zimewekwa juu zaisi
Pia maeneo yametengwa
kwa wavuta sigara ili wasitangamane na wasiovuta
Kuelimisha jamii
madhara ya sigara na mbinu za kujiepusha na matumizi;serikali pia imepiga hatua
kuona kuwa elimu inatolewa mara kwa mara kwa jamii.
Endapo suluhu hizi zitakuwa na mafanikio,basi
ifikapo mwaka wa 2030 idadi ya wanaoadhiriwa na hali hii itapunguka kwa kiwango
cha theluthi moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni