Chombo cha kuchoma taka ya matibauLengo
la kutafuta matibabu hospitalini ni kwa minajiri ya kupata afya bora.Lakini je
taka za matibabu zina madhara gani ya kimazingira na fya ya mwanadamu?
Tafiti zinaonyeza kuwa asilimia 85 ya taka ya matibabu haina madhara ya kiafya au mazingira;lakini 15%(asilia kumi na tano) ni taka iliyo na kemikali zenye sumu.Hivyo basi ni jukumu la wanaozoa taka za matibabu kuhakikisha wameitumia mbinu zinazofaa kuchoma jinsi inayofaa.
Utupaji taka ya matibabu una changamoto zake.
Huku hospitali zikiongezeka kila uchao, utupaji na uchomaji taka ya matibabu imekuwa ni shida hasa katika harakati za kuhifadhi afya na mazingira.Ni hospitali chache ambazo zina chombo maalum cha kuchoma taka ya matibabu.Baadhi ya hospitali za kibinafsi na pia zile za umma zinatupa taka ovyo ovyo bila kujali maslahi ya wananchi.
Ni jukumu la serikali na pia wadau katika sekta ya mazingira,kuhakikisha sera simetungwa.
Pia mikakati au namna ya kuwa surutisha wafanyikazi wa afya
ya umma kuhakikisha afya na mazingira yamehifathiwa ipasavyo iwepo.
Itakuwa ni hatari kutupa taka za aina hii ovyo kwa maana zina kemikali ya sumu ambayo inadhuru afya ya wanadamu.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani(WHO), shindano billioni kumi na sita hutumiwa katika hospitali kote duniani,lakini sio zote zinazotupwa au kuchoma kamainavyostahili.
Kisa cha hivi karibuni ni huko Meru ambako hospitali ilitupa taka za hospitali hiyo na kuchomea kwa sehemu iliyo wazi;huku ikihatarisha maisha ya wananchi.
Itakubukwa kuwa hii ni hospitali ya umma.Jambo la kushangaza ni kuwa hawana chombo cha kuchomea taka ambacho ni lazima kila hospitali iwenacho au ionyeshe jinsi itakavyo haribu taka za matibabu kabla kupata leseni kutoka kwa shirika la kuhufadhi mazingira.
Kulingana na sheria za kiafya ni sharti taka za matibabu ziwekwe kwenye karatasi ya kijano;taka mbayo hayana madhara au hatari na nyekundu ;taka amayo ina kemikali za sumu.
Pia sinastahili kutibiwa kabla zichomwe au ziharibiwe.Endapo hospitali haina chombo cha kuchoma taka inweza kukodisha kwa hospitali zingine zilizo karibu.Hii imekuwa ni changemoto ambayo isipotatuliwa kwa haraka basi maisha ya wananchi itakuwa hatarini.
Aina ya taka ambazo ni hatari
Taka inayoabukiza kama vile damu au uchafu kutoka kwa wagonjwa walio na maradhi ya kuabukiza.Endapo hazitaharibiwa ipasavyo basi maradhi wanaweza kuwapata au kuabukiza watu
·
Nyama au vipande vya nyama
vinavyotolewa kufanyiwa tafiti vinapotupwa bila mwelekeo vina hatarisha maisha
ya watu na pia wanyama.
·
Taka yenye makali
kama vile shindano,wembe zinapotupwa ovyo zinaweza kujeruhi na kusababisha
majeraha makali
·
Kemikali za sumu
zinazo tumiwa kwenye mahabara pia zina adhari.· Dawa
na chanjo ambazo muda wa kutumia umeisha
Taka isiyo na madhara: taka ambazo
hazihusishi na hatari yoyote ya kibaiolojia, kemikaliau ya kimwili.
Sehemu ambazo huchangia ongezeko la taka
-Hospitali,zahanati na sehemu zinazojihuzisha na afya ya umma.
-Sehemu zinazofanyiwa tafiti kama
vile maabara
-Sehemu zakuhifadhia damu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni