Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo. Visababishi na ukubwa tatizo Saratani ya thyroid huwapata watu wa umri mbalimbali, kuanzia watoto mpaka watu wazima. Watu waliowahi kupigwa mionzi sehemu ya mbele ya shingo wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya saratani. Kadhalika watu wazima ambao waliwahi kupigwa mionzi kipindi cha utotoni nao pia wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya thyroid hata kama hawakuwahi kupata tatizo hilo wakati wanakua. Tiba ya mionzi maeneo ya shingoni ilikuwa ikitumika sana zamani kwenye miaka ya 50 mpaka 60 kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa tezi ya thymus, mafindofindo (tonsils), au baadhi ya magonjwa ya ngozi. Hata hivyo ni nadra sana kwa tiba hii kutumika katika zama hizi. Vihatarishi vingine vya saratani ya tezi ya thyroid ni pamoja na kuwepo kwa historia ya tatizo hili miongoni mwa wanafamilia na kuw...
Machapisho
Marehemu Michuki aombolezwa
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Marehemu John Michuki Wakenya wa tambaka mbalimbali waendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri wa mazingira John Njoroge Michuki aliyefariki dunia jumanne,kwa mstuka wa moyo, katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan. Akizaliwa 1932 katika kitongoji cha Jimbo la Kagema katika wilaya ya Muranga. Alipata masomo yake ya upili katika shule ya Mangu pamoja na rafikiye wa dhati rais Mwai Kibaki. Aliendelea na masomo yake katika chuo cha Worcester,Oxford huko Uingereza. Wengi wamemtaja michuki kama kiongozi mchapa kazi , aliyedumisha nidhamu ya hali ya juu kazini na aliyejitolea kwa kila alilofanya. Rais Mwai Kibaki ambaye ni rafikiye marehemu alisema kuwa Michuki alikuwa mwanasiasa hodari,aliyetekeleza kazi yake kwa uadilifu.Pia mwana biashara stadi. Kulingana na mhariri wa habari wa kujitengemea Onesmus Kilonzo Michuki atakubukwa kwa kulainisha sekta ya matatu,na uhifadhi wa mto Nairobi miongoni mwa mengine “kila ofisi aliohudumia ilipata ufa...
WHO yasema depo provera ni salama
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Shirika la Afya Duniani ( WHO) limeondolea lawama shindano ya Depo Provera kuwa inachangia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU). Shirika hili (WHO) linahakikishia wanawake wanaotunia aina ya uzazi wa mpango wa homoni kuwa hakuna hatari ya kutumia aina hii, kama ilivyo daiwa hapo wali. Hata hivyo (WHO) imeonya kuwa ni aina moja pekee ya uzazi wa mpango inayozuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi - kondomu au mpira. Huku likisisitiza kuwa ni muhimu kwa wale wako kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi kuchukua tahadhali. Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani utafiti unafanywa kwa nia ya kuhakikisha malengo ya milenia ya afya imefikiwa. Uvumbuzi kuwa utumiaji dawa ya upangaji uzazi ya homoni ijulikanayo kama Devo Provera unachangia ongezeko la maabukuzi ya ugonjwa hatari wa ukimwi, miezi michache iliyopita, uliwaacha wanawake wengi na hofu na husuni tele. Inakadiriwa kuwa takribani millioni 12 ya wanawake wenye um...
Saratani ya tezi kibofu cha mkojo (Prostate)
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Saratani ya tezi kibofu ni ugonjwa ambao huwa kati ya wanaume.kama aina nyingine za saratani, inapogunduliwa mapema inakuwa ni rahisi kutibiwa. Zaidi ya hayo, walio hatarini ya kuambukizwa Ugonjwa huu ni wanaume walio na umri wa miaka 55 na zaidi. Hivi majuzi, ugonjwa wa saratani umetia wengi kiwewe.Siku baada ya siku kuna habari kuwa mtu fulani ana ugonjwa wa saratani.Waume kwa wanawake,vijana kwa watoto wote wako hatarini ya kuabukizwa ugonjwa huu. Watafiti bado hawajapata uvubuzi ni nini haswa inayo sababisha ugonjwa huu hatari. Hata hivyo inakisiwa kuwa mazingira tunayoishi, kwa njia moja ua nyingine yanachangia kuwepo kwa maradhi haya. Hapa nchini Kenya waziri wa afya ya umma Mheshimiwa Beth Mugo alitangaza kuwa amegunduliwa kuugua saratani ya matiti na kwa sasa anaendelea na matibabu huko Marekani. Waziri Mwenzake, Prof. Anyang Nyongo pia aligunduliwa kuugua saratani ya tezi kibofu.Kwa bahati nzuri, iligunduliwa mapema na baada y...
kongamano la uzazi mpango Dakar,Senegal
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kongamano kuhusu afya ya uzazi yaanza leo jijini Dakar nchini Senegal. Mkutano huu unafanyika huku karibu watu millioni 900 kote duniani wakikumbatia uzazi wa mpango. Hata hivyo, sio wote wanaoweza kufanya uzazi wa mpango wakati wanapotaka kufuatia changamoto kadha wa kadha. Mkutano huu utawajumuisha watafiti wa afya,madaktari na wadau wengine katika sekta ya afya. Kufanyika kwa mkutano huu katika Afrika Magharibi,ni jambo la muhimu ikifahamika kuwa nchi za Afrika Magharibi zinaongoza kwa idadi ya watu kwani mpango wa uzazi ungali haujapewa kipao mbele. Pia kupata hutuma ya uzazi wa mpango ni shinda. Inaaminika kuwa wazazi wengi ambao wangependa kupanga uzazi wanasubuka sana.Hata kabla wapate huduma hiyo muhimu wanagundua kuwa ni wajawazito.Idadi ya wanandoa walio kwenye hali hii ni zaidi ya millioni 215 kote duniani. Uzazi wa mpango u nawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya ...
FGM (ukeketaji) Kenya
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Ukeketaji Ni asubuni na mapema,jua linapoanza kuchomoza,katika kijiji kimoja katika Mkoa wa Mashariki. Kundi la akina mama linafululiza hadi kwa mama mwenzao, huku wakiimba nyimbo za kitamaduni. Kisa na maana ; hajakeketwa. Nia yao haswa ni kutumia nguvu kumkeketa kwani ni kero kwa wanawake wa kijiji chao. Kulingana na mila na desturi ya jamii hiyo ni sharti mwanamke akeketwe anapokaribia kuvunja ungo.Lakini kwa mama Matani* aliolewa kabla hajakeketwa. La kuhuzunisha ni kwamba yeye ni mjamzito na kitendo hiki kinaweza kuhatarisha maisha yake. Kwa bahati nzuri,anaepuka gadhabu ya akina mama hao baada ya chifu wa kijiji hicho kuingilia kati.Wanarudi makwao huku wakiapa kumuadhibu mama Matani* baadaye. Wakati wakujifungua ,yule mama hana budi kuwaita baadhi ya wale wanawake kumsaidia kujifungua. Sasa wanapata nafasi ya kumkeketa katika ile harakati ya kuzaa.Anajifungua mtoto na afya zake,anakeketwa na sasa ni mama kamili…..unyama ulioje? Hii si hadithi bali ndivyo hali ilivyo katika ...