Wangari maathai road
Msitu wa karura ulimpa umaarufu Marehemu Prof. Wangari Maathai Juhudi za hayati Wangari Mathaai za kuhifadhi mazingira zatambuliwa na jimbo la jiji la Nairobi na kumtunuku kwa kubadilisha njia ya Limuru na kuipa jina mpya ya Wangari Mathaai. Maathai alikuwa mwanamazingira maarufu aliyejitolea mhanga kuhakikisha wanyakuzi wa ardhi walikabiliwa vilivyo. Barabara ya Limuru inapitia kwenye msitu wa karura na pia ni njia ambayo inaelekea kwenye makao makuu ya uhifadhi wa mazingira ya Umoja wa Mataifa,Nairobi. Zaidi ya hayo,Kuna bustani nchini Peru ambayo pia imepewa jina la Wangari Maathani.Na pia Marekani na Japani. Mama Mathaai aliaga dunia miaka minne iliyopita baada ya kuugua saratani ya mfuko wa uzazi(Ovarian Cancer) Marehemu Maathai alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004 na kuwa mwanamke wa kwanza mwafrika, mkenya wa kwanza na mwanamazingira wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo. Umaarufu wa Mathaai ulitokana na ari yake y...