Machapisho

Shirika la Afyan duniani linafanya kikao hii leo mjini Geneva kujadili maswala ya COVID 19 WHO assembly Mkutano huu wa siku mbili unaendelea huku Taiwan ikipinga hatua ya kutengwa katika vikao vya baraza la shirika la afya duniani WHO huku ikisema itakuwa ni hasara kutohudhuria kikao hiki ikizingatiwa kuwa imefanikisha juhudi zake za kukabiliana na virusi vya Corona. Taiwan na nchi nyingine kadhaa zimelitaka shirika hilo kuialika katika mkutano huo unaofanyika moja kwa moja kupitia mitandao. Haya yanajili huku uhusiano baina ya Uchina na marekani ukiendelea kuzorota. Hapo awali Marekani ambaye ni muhisani mkuu wa WHO ilitangaza kusimamisha  msaada wake wa kifedha huku nchi hiyo ikilaumu Shirika hilo kwa kushirikiana na kuipendelea Uchina katika harakati zake za kukabiliana na janga la COVID 19.  Waziri wa Afya na Ustawi wa Taiwan, Chen Shih-Chung amenukuliwa akilaumu hatua ya kutoshirikishwa kwenye baraza la afya la umoja wamataifa. Taiwan ...

Antonio Guerres -Corona

Corona au COVID-19. Huku siku ya uhuru wa vyombo vya habari ikiadhimishwa tarehe 3 Mei kote duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wanahabari na wafanyakazi katika vyombo vya habari wana majukumu muhimu katika kusaidia ulimwenguni kusambaza habari ipasavyo kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Alisema ni vema serikali kuwapatia nafasi na uhuru waandishi kutekeleza majukumu yao bila hofu,kuingiliwa au kutishiwa. Siku ya uhuru was waandishi was habari huadhimishwa kila mwaka; maudhui ya mwaka huu ikiwa,uandishi wa habari bila uoga wala upendeleo,. Tangu mlipuko was COVID 19 wanahabari wamejipata pambaya n'a selikali tofauti kufuatia j'insiste wanavyo ripoti maambukizi ya Corona.  Hivi majuzi Tanzania ilistumu vikali habari kuwa kuna idadi kubwa ya maambukizi nchini humo.  Serikali ya Kenya piano ili kashfu taarifa kuwa idadi ya maambukizi ni zaidi kuliko inavyotangazwa n'a selikali. Wanahabari pia wanahitaji kulindwa wanapoen...

Augustine Philip Mahiga

Picha
Aliyekuwa Waziri wa Sheria, Tanzania, Augustine Philip Mahiga afariki dunia ghafla huko Dodoma. Rais Pombe Maghufuli ametangaza .

Silas Njiru-Askofu

Picha
Askofu mstaafu Silas Njiru Afariki dunia Virusi vya Corona vimepokonya kanisa katoliki na Kenya kwa jumla Askofu Mstaafu wa Jimbo la Meru,Silas Njiru . Askofu Njiru alifariki mapema Jumanne nchini Italia baada ya kuambukizwa Covid-19. Askofu wa Meru Salesius Mugambi ambaye alichukua hatamu za uongozi wa jimbo hilo baada ya kustaafu kwa marehemu, alisema Askofu huyo mstaafu alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Rivoli ambapo alikuwa amelazwa kwa siku tatu. Hapo awali Asofu wa jimbo la Embu kupitia ujumbe kwenye mtando, aliomba wakristo kumuombea Marehemu kwani alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi .   Alikuwa miongoni mwa mapadre   watatu walioambukizwa virusi vya Corona kwenye makao yao. Marehemu alikuwa akikaa katika nyumba ya Mtakatifu Joseph Allamano huko Alpignano, Turin, Italia tangu kustaafu kwake. Alizaliwa Mwezi 1928 katika kijiji cha Kevote, Kaunti ya Embu. Alihudhumu katika jimbo la Meru kwa muda mrefu zaidi,pia amekuwa Padre kwa miaka...

COVID 19 Kenya

idadi ya maambukizi yaongezeka kenya Idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa COVID 19 imefikia 374 baada ya watu wengi 11 kupatikana na maambukizi. Kati ya visa 11 mpya, saba ni kutoka Jimbo la Nairobi na nne kutoka Mombasa. Walioambukizwa wakiwa kati umri wa   miaka mitatu na 70. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za   Wizara ya Afya ya Kenya .   Kaimu Katibu Mkuu wa Afya Rashid Aman,amesema   idadi ya watu wote waliopona sasa wamefika 124 baada ya watu wengine 10 kuopona baada ya masaa ishirini na nne. Kuna visa vipya katika maeneo manne Nairobi,   manne yalikuwa kutoka Kawangware, na mengine kutoka maeneo ya Eastleigh, Manji na Kaloleni. Dkt Aman ametowa wito kwa maafisa wa polisi kuhakikisha harakati na mbinu   za kuigia ndani na nje ya kaunti hizi mbili zinazingatiwa   kuzuia kuenea kwa virusi hivyo ambavyo vimewaambukiza zaidi ya watu milioni 3 na kuwauwa watu 212,337 ulimwenguni. Wizara ilifafanua zaidi kwamba baa zitab...

Malaria 2020

Siku ya malaria yaadhimishwa huku maambukizi  ya janga la Corona yakiendelea kuongezeka.
COVID 19 Maambukizi yaongezeka Tanzania Idadi ya wagonjwa wa COVID 19 imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini Tanzania. Hii leo visa 30(thelathini) vimeripotiwa huku idadi ya maambukizi ikifika 284. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa litoa taarifa ya maambukizi zaidi   wakati wa maombi ya taifa   jijini Dar es Salaam leo.  Majaliwa alisema kufikia jana   wagonjwa 256 wanaendelea vizuri huku saba wakiwa kwenye uangalizi maalumu. Idadi ya waliofariki ni 10 huku 11 wakipona. Waziri Mkuu ,Bw. Majaliwa amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona vimedhibitiwa . Amesema serikali inatoa eimu kwa umma jinsi ya kujikinga,kamati ya kitaifa imeundwa ili kufuatilia hali ya ugonjwa nchini na pia timu ya wataalamu wa afya imeundwa ili kushughulikia swala hili. Bw.majaliwa amewataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya wataalamu wa afya na serikali ili kuepuka athari Zaidi ...