idadi ya maambukizi yaongezeka kenya
Idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa COVID 19 imefikia 374 baada ya watu
wengi 11 kupatikana na maambukizi.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa za Wizara
ya Afya ya Kenya .
Kaimu Katibu Mkuu wa Afya Rashid
Aman,amesema idadi ya watu wote waliopona
sasa wamefika 124 baada ya watu wengine 10 kuopona baada ya masaa ishirini na
nne.
Kuna visa vipya katika maeneo manne Nairobi, manne yalikuwa kutoka Kawangware, na mengine
kutoka maeneo ya Eastleigh, Manji na Kaloleni.
Wizara ilifafanua zaidi kwamba baa zitabaki kufungwa . wamiliki wa mikahawa
waliruhusiwa kufungua .
Kesi 374 za Covid-19 nchini zimesambaa kati ya Homa Bay (1), Kajiado (3),
Kakamega (1), Kiambu (5), Kilifi (9), Kitui (2), Kwale (1), Mandera (8),
Mombasa (97), Nairobi (241), Nakuru (2), Siaya (2) na Uasin Gishu (1).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni