Mwana Nzeki ni shujaa,hakika shujaa ametuaga.
Aliyekuwa Askofu mstaafu wa Katoliki jimbo la Nairobi alikuwa shujaa hakika.
Alipokuwa Askofu wa Jimbo la Nakuru alishuhudia mauaji ya kikabila jambo
ambalo lilimghadhabisha hadi akakemea serikali iliyoongozwa na Mwenda zake Rais
Daniel T Moi.
Iwe ni siasa au uongozi mbaya wa kisiasa yeye hakusita kukosoa
serikali na wahusika .
Hakuogopa chochote,aliamini anafanya kazi ya Mungu na alifanya
kwa moyo wake wote.
Ilikuwa ni husuni na majonzi hiyo jana baadha ya kutangazwa kwa kifo chake .Kiongozi
wa kanisa Katoliki nchini Kadinali John Njue ,ndiye aliyetangazwa kifo chake.
Kulingana na taarifa ya kadinali Njue, lifariki jana asubuhi
katika makao ya viongozi wastaafu wa kanisa Katoliki jijini Nairobi baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Rais Uhuru,alitoa rambirambi zake huku akimtaja Askofu huyo kama
kiongozi shujaa wa kidini aliyejawa na upendo .
Makamu wa rais William Ruto,Kiongozi wa ODM ,Raila Odinga na
viongozi wengine wa kisiasa walimtaja Marehemu Askofu kama mtetezi wa wanyonge
aliyepigania haki zao.
Alizaliwa mwaka wa 1931, Mwala kaunti ya Machakos. Baada ya
kukamilisha masomo ya shule ya msingi alijiunga na mafunzo ya upadre katika
seminari ilioko eneo la Kiserian, kaunti ya Kajiado.
Mola ailaze roho yake palipo watakatifyu wake…Amina
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni