MAMA GETRUDE RWAKATARE AFARIKI DUNIA
Mawanawe Muta Rwakatare,alitoa taarifa ya kifo cha mamake.Anasema Askofu alikuwa na matatizo ya moyo na alifariki hospitalini ambapo alipelekwa baada ya kuugua ghafla.
Alikuwa
ni mtumishi wa Mungu,Mbunge maalum na mwanabiashara mashuhuri nchini Tanzania
Askofu Daktari mama Rwakata alikuwa na
maneno na sauti nyororo ya kumtoa nyoka
pangoni.
Nakumbuka wakati mmoja nilipozuru Dar es
salam ,marafiki wangu wakanikaribisha kutembelea kanisa la Mlima wa moto pale
mikocheni B.
Nilipoketi na kusikiriza mafunzo/mahubiri yake mama Rwakatare nilijihisi kama nimezaliwa tena kiroho, tangu wakati huo nilipenda kusikiliza mahubiri yake kwenye televisioni .
Alikuwa kwenye mstari wa mbele kwenye
maswala ya usawa wa jinsia hasa maswala na kina mama na maendeleo.
Mchungaji Rwaktare alizaliwa Kilombelo
,huko morogoro, akasomea Korogwe na baadaye akaenda nchini Kenya kwa masomo ya
Chuo kikuu katika Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Alikuwa ni msomi aliyekuwa na hamu ya
kuona kila mtanzania amepata elimu ya hali ya juu.
Hii ilipelekea yeye kuanzisha
shule za St Mary ambapo watanzania wengi walio kwenye nyaja mbalimbali nchini
wamepitia.
Fahari na heshima ya mwanaume alisema ni
kazi
Mola ailaze roho yake palipo watakatifu
wake …Amina
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni