Huku idadi ya maambukizi ya virusi vya
Corona yakiongezeka hadi 81,Wakenya wa kwanza kupatikana na virusi hivyo wamepona.
Brenda Cherotich na Brian Orinda walikuwa wa kwanza kupatikana na virusi vya Corona.
Wamekutoka hadharani kuwashauri wakenya kuwa wasiwe na hofu kwani kuna kupona hata baada ya maambukizi ya Corona.

Hakika kwao Brenda na Brian ni faraja baadha ya dhiki .
Brenda aliwasili kenya kutoka Marekani
ambao alizuru,kupitia uingereza na anadhani kuwa aliambukizwa virusi vya Corona
katika shughuli zake za usafiri.
Aliporejea kenya alikohowa kwa siku tatu
na kuamua kujipeleka kwenye kituo cha afya ,alipowekwa katika chumba ambach wagonjwa wa Coriona wanamoka wakipokea
matibabu. Rafikiye Brian aliyetangamana naye pia aliambukizwa.Wote kwa sasa wamepona na wanashukuru kwani wahudumu wa afya waliwashughulikia ipasavyo.
Wakati huu huu Rais Uhuru Kenyatta amempongeza
Brenda kwa ukakamavu wao.
Rais ametaka wakenya kuiga mfano wa Brenda
na Brian ,kwa kutembele vituo vya afya wanapojihisi kuwa na dalili za Virusi
vya corona.
Kenya imeweka mikakati kambambe
kukabiliana na Corona hasa swala la kunawa mikono na kutoa matangazo ya
kuelimisha wakenya kuhusu janga la Corona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni