chimbuko la Virusi vya Corona
Shirika
la Afya Duniani, WHO limesema kuwa hakuna ushahidi kuwa wa virusi vya Corona vilitengenezewa kwenye
maabara.
Hata
hivyo Msemaji wa shirika hilo, Fadela
Chaib amesema ushahidi uliopo unadhihirisha kuwa virusi vya corona vilitoka kwenye wanyama
nchini China mwishoni mwa 2019.
Akihutubia mkutano wa waandishi habari mjini Geneva, alisema
kuna uwezekano mkubwa vilitoka kwenye popo.Zaidi ya hayo,anasema haijabainika
ni vipi virusi hivyo vilitoka kwenye popo na kuingia kwa binaadamu.
Hapo awali, Rais wa Marekani Donald Trump
alisema kuwa serikali yake inajaribu kubaini kama virusi hivyo vilitengenezwa
kwenye maabara katika mji wa Wuhan nchini China, ambako janga la virusi vya
corona lilianzia Desemba mwaka uliopita.
Kumekuwa
na maoni na misimamo tofauti kuhusu ni jinsi gani virusi vya Corona vilikotoka
huku wengi wakijadili kuwa vilitoka kwa wanyama huku wengine wakisema
vilisababishwa au vilitengenezwa kwenye maabara.
Kulingana
na tafiti za wataalam wa afya huko China baada ya mripuko awamu ya kwanza,iligunduliwa
kuwa watu 27 kati ya wagonjwa 41
waliokuwa wamelazwa hospitali katika awamu ya kwanza ya mlipuko corona waliwahi
kufika katika soko la samaki la Huanan
Hivyo basi matokeo ya tafiti inadokeza uwezekano wa
Matokeo ya maambukizi yalianza kusambaa kutoka soko hilo.
Isitoshe, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
maambukizi yalitoka kwa wanyama kabla ya
kumuingia binadamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni