Takwimu zinaonyesha ongezeko ya
maambukizi hadi milioni 2 kufikia sasa,huku vifo vikiwa elfu 131.
Marekani na mataifa ya Uropa yanaongoza
katika vifo na maambukizi duniani.
Ikifuatiwa na Italiano na vifo 21,645,Uhispania
nayo ni ya tatu na maafa ya kiwango cha 18,579.
Ufaransa inachukua nafasi ya nne na vifo Zaidi ya elfu 17 huku Uingereza ikiwa
ya tano na vifo elfu 12.
Tarifaa hii inatolewa siku moja baada ya
Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha mswada wa fedha kwa Shirika la Afya
Duniani kwa kile alichokitaja kama kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maambukizi
ya Corona na pia kuelekeza juhudi zake nyingi Uchina katika shughuli za
kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom,
amesema kuwa nimatumaini yake Marekani ataendelea kuwa mshirika wa karibu wa
shirika hilo kama ambavyo amekuwa kwa muda mrefu.
Mataifa tajiri duniani G20 yametangaza kuahirisha malipo ya madeni
yake kwa mataifa yaliyo na mikopo kwa muda wa mwaka mmoja.
Nchi ya Denmark na Ugeremani masomo
yamerejea huku mataifa ya utaliano na uhispania wakirejea kazi kwa baadhi ya
kampuni.
Hatua kali zimewekwa kwa wale watakao
kiuka maagizo ya serikali.
Pia usafiri wa sehemu za majimbo
zimekatizwa na wanaoishi miji ilioko karibu na jiji la Nairobi wanapaswa kuwa
nyumbani ifikapo saa moja kamili.
Idadi ya maambukizi Kenya imefika 225
huku vifo vikiwa kumi hadi sasa.
Jimbo la Nairobi linaongoza katika
maambukizi ya watu 163,Mombasa ikifuata na watu 36 Kilifi ikiwa na watu kumi
huku mandera ikiwa na watu sita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni