Jumatano, 22 Aprili 2020



COVID 19 Maambukizi yaongezeka Tanzania

Idadi ya wagonjwa wa COVID 19 imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini Tanzania.
Hii leo visa 30(thelathini) vimeripotiwa huku idadi ya maambukizi ikifika 284.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa litoa taarifa ya maambukizi zaidi  wakati wa maombi ya taifa  jijini Dar es Salaam leo.

 Majaliwa alisema kufikia jana  wagonjwa 256 wanaendelea vizuri huku saba wakiwa kwenye uangalizi maalumu.

Idadi ya waliofariki ni 10 huku 11 wakipona.
Waziri Mkuu ,Bw. Majaliwa amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona vimedhibitiwa .
Amesema serikali inatoa eimu kwa umma jinsi ya kujikinga,kamati ya kitaifa imeundwa ili kufuatilia hali ya ugonjwa nchini na pia timu ya wataalamu wa afya imeundwa ili kushughulikia swala hili.
Bw.majaliwa amewataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya wataalamu wa afya na serikali ili kuepuka athari Zaidi kwa taifa
Tanzania imeendelea kutangaza maambukizi Zaidi katika Afrika Mashariki baadaya Kenya.
Hapo awali,Rais wa Tanzania ,Pombe magufuli alitangaza siku tatu za maombi kufuatia mripuko wa Corona.
Hii leo viongozi 
wa madhehebu mbalimbali ya kidini walikongamana kwa maombi maalumu kwenye mapambano dhidi ya janga la Corona 
Viongozi hao hawakuachwa nyuma katika harakati za kujikinga na virusi.walifalia barakoa na kuketi umbali wa zaidi ya mita moja kama inavyopendekezwa na wataalam wa afya wa WHO duniani.
      Kenya yaripoti visa 7(saba) leo
Kenya imeripoti visa zaidi leo yaani watu 303 sasa wameambukizwa virusi vya COVId 19.
Kufuatia ongezeko hili, Waziri wa Afya ,Mutahi Kagwe amesitisha usafiri wa hewa na barabara kuingia na kutoka jimbo la mandera ambapo maambukizi yameendelea kuongezeka kwa kasi.
Anasema hatua hii imechukuliwa ilikuepuka maambukizi baina ya jamii .






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni