Virusi vya Corona vimepokonya kanisa katoliki na Kenya kwa jumla Askofu
Mstaafu wa Jimbo la Meru,Silas Njiru .
Askofu Njiru alifariki mapema Jumanne
nchini Italia baada ya kuambukizwa Covid-19.
Askofu wa Meru Salesius Mugambi ambaye
alichukua hatamu za uongozi wa jimbo hilo baada ya kustaafu kwa marehemu, alisema
Askofu huyo mstaafu alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Rivoli ambapo
alikuwa amelazwa kwa siku tatu.
Hapo awali Asofu wa jimbo la Embu kupitia
ujumbe kwenye mtando, aliomba wakristo kumuombea Marehemu kwani alikuwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi .
Marehemu alikuwa akikaa katika nyumba ya
Mtakatifu Joseph Allamano huko Alpignano, Turin, Italia tangu kustaafu kwake. Alizaliwa
Mwezi 1928 katika kijiji cha Kevote, Kaunti ya Embu.
Alihudhumu katika jimbo la Meru kwa muda mrefu zaidi,pia amekuwa Padre kwa miaka zaidi ya sitini.
Mola ailaze roho pema peopni.
- Ugonjwa wa Corona na walio kwenye hatari
- Watu wenye umri wa miaka sitini na zaidi
- Walio na ugonjwa wa kisukari
- Ugonjwa wa moyo baadhi ya maradhi mengine.
Pamoja tuangamishe Corona
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni