COVID 19 Maambukizi yaongezeka Tanzania
Hii leo visa 30(thelathini) vimeripotiwa huku idadi ya maambukizi
ikifika 284.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa litoa taarifa ya maambukizi
zaidi wakati wa maombi ya taifa jijini Dar es Salaam leo.
Majaliwa alisema kufikia jana wagonjwa 256
wanaendelea vizuri huku saba wakiwa kwenye uangalizi maalumu.
Idadi ya waliofariki
ni 10 huku 11 wakipona.
Waziri Mkuu ,Bw. Majaliwa amesema
serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya
virusi vya Corona vimedhibitiwa .
Amesema serikali
inatoa eimu kwa umma jinsi ya kujikinga,kamati ya kitaifa imeundwa ili
kufuatilia hali ya ugonjwa nchini na pia timu ya wataalamu wa afya imeundwa ili
kushughulikia swala hili.
Bw.majaliwa
amewataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya wataalamu wa
afya na serikali ili kuepuka athari Zaidi kwa taifa
Tanzania imeendelea
kutangaza maambukizi Zaidi katika Afrika Mashariki baadaya Kenya.
Hapo awali,Rais wa Tanzania ,Pombe
magufuli alitangaza siku tatu za maombi kufuatia mripuko wa Corona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni