Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2014

Dr Umar Khan afariki

Daktari mashuhuri wa ebola amefariki. Dk. Sheik Umar Khan   Alijitolea  mhanga kuwatibu  walio ambukizwa  Virusi vya ebola. Hata hivyo ajari haina kinga katika harakati ya kuhakikisha kuwa amewatibu wagonjwa, alipata Virusi vya ebola wiki moja iliyopita. Hivi majuzi kwenye mahojiano na wana Habari, Dk.Umar alisema yeye kama mwanadamu yeyote anathamini uhai na alihofia uhai wake lakini hangeacha kutekelezwa wajibu wake. Mola ailaze roho yake mahali pema peponi. Idadi ya vifo nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia Inakisiwa kuwa 672 kutoka Februali mwaka huu.

cancer conference,windhoek

Picha
                                        Kongamano la saratani  Mkutano kuhusu ugonjwa hatari wa saratani umeanza hii leo  mjini Windhoek,Namibia. Mkutano huu hulifunguliwa na rais Hifikepunye Pohamba huku akisema ni muhimu kwa umoja wa Afrika na pia mataifa tofauti Afrika kutafuta binu na mikakati ya kuangamisha saratani. Mada ya mkutano huu ni kuendelea na mikakati ya kutambua na kutibu   saratani ya shingo ya uzazi yaani cervical cancer  imekuwa donda ndungu kwa wanawake .Saratani ya matiti pia inaenea kwa haraka barani Afrika. Malengo mengine ni kutafuta binu ya kuzuia  kenea kwa saratani ya shingo ya uzazi ifikapo mwaka wa 2030. Rais Pohamba alilalama kuwa zaidi ya watu millioni  28 hufariki kutokana na maradhi ya saratani kila mwaka jambo...

AIDs conference

Picha
Kongamano la kimataifa  kuhusu  ukimwi latia nanga  ,huku washiriki wakitoa heshima kwa wenzao waliofariki kwenye ajari ya ndege ya Malaysia.  Husuni ilitanda kote kwenye ukumbi huyo wa mikutano. Hakika kifo cha wataalamu hao sita  ni pigo kwenye kongamano hilo na ulimwengu kwa jumla. Aliwataja kama mashujaa na watafiti  yalihobea katika nyanja ya utafiti na afya. Rais wa Shirika la Ukimwi Duniani, Francoise Barre-Sinoussi alisema hata baada ya mkasa huo washiriki wataendelea kufanya vikao wakiwa na lengo la  kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi.  Shirika la Afya Duniani(WHO) pia limepata pigo baada ya msemaji wake Glenn Thomas ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mwadishi wa Shirika la Utangazaji la BBC . Glenn raia wa uingereza alipenda sana kuangazia maswala ya afya na alitumika katika shirika la WHO kwa miaka kuni.Kwa hakika viti vyao vilibaki wazi huku  vitambulisho vyao vikibaki mezani huku  majukumu waliotengewa ka...

Aids2014..ukimwi melbourne

Picha
                                         MKUTANO KUHUSU UKIMWI 20                                           Mkutano unatarajiwa kuanza jumapili mjini Melbourne, Australia.watalaamu wa afya na watafiti wa makali ya ukimwi duniani kote wamealikwa.    Habari njema ni kuwa maambukizi ya ukimwi imepunguka kote ulimwenguni . Shirika la Ukimwi duniani linabaini   kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na ukimwi duniani vimepungua kwa kasi mwaka 2013 sawa na asilimia 11.8% ndani ya mwaka mmoja. Zaidi ya hayo UNAIDS inasema kwamba lengo l...

Joep Lange

Picha
Jeop Lange mtafiti wa tiba ya makali ya ukimwi aaga dunia. -Sekta ya afya na tiba, na dunia kwa jumla inaomboleza kifo za Jeop Lange, mtafiti wa tiba ya makali ya ukimwi dunia. Mtafiti stadi wa afya duniani ni miongoni mwa  abiria waliofariki baada ya ndege ya Malaysia,waliokuwa wakisafiria, kuanguka huko Ukraine. Joep Lange alikuwa mwanasayansi mashuhuri ambaye pamoja na watafiti wenzake lifanya juu chini kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi duniani.  Lange Pia ni raia wa Uhoranzi. Lange alikuwa profesa na mkurugenzi kuu wa kitengo cha afya na utabibu katika chuo kikuu cha Amsterdam,uholanzi.Amekuwa katika mstari wa mbele kutafuta tiba ya makali  ya ukimwi kwa miaka thelathini.Mkewe pia alifariki kwenye ajari hiyo. Mtafiti kutoka Amerika,Dkt Rick Elion alimtaja Lange kama mtu mwenye roho ya dhahabu,mkarimu na mwenye bidii kama ya mchwa. Inakisiwa baadhi ya  abiria kwenye ndege hiyo  ya Malaysia  walikuwa wataalamu wa afya na watafiti ...