Jumatatu, 21 Julai 2014

cancer conference,windhoek

 







                                      Kongamano la saratani 


Mkutano kuhusu ugonjwa hatari wa saratani umeanza hii leo  mjini Windhoek,Namibia.
Mkutano huu hulifunguliwa na rais Hifikepunye Pohamba huku akisema ni muhimu kwa umoja wa Afrika na pia mataifa tofauti Afrika kutafuta binu na mikakati ya kuangamisha saratani.


Mada ya mkutano huu ni kuendelea na mikakati ya kutambua na kutibu   saratani ya shingo ya uzazi yaani cervical cancer  imekuwa donda ndungu kwa wanawake .Saratani ya matiti pia inaenea kwa haraka barani Afrika.



Malengo mengine ni kutafuta binu ya kuzuia  kenea kwa saratani ya shingo ya uzazi ifikapo mwaka wa 2030.

Rais Pohamba alilalama kuwa zaidi ya watu millioni  28 hufariki kutokana na maradhi ya saratani kila mwaka jambo ambalo nila kuhuzunisha.

Mkewe Rais wa kenya Margaret Kenyatta ni miongoni mwa  wake wa marais wanane wanaohudhuria  kongamano hii ya siku tatu.
 


Bi Kenyatta amekuwa mstari wa kwanza kama mama wa taifa kuangamizia na kupigia debe maswala ya afya na akina mama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni