Kongamano la kimataifa kuhusu ukimwi latia nanga ,huku washiriki wakitoa heshima kwa wenzao waliofariki kwenye ajari ya ndege ya Malaysia.
Husuni ilitanda kote kwenye ukumbi huyo wa mikutano.
Hakika kifo cha wataalamu hao sita ni pigo kwenye kongamano hilo na ulimwengu kwa jumla. Aliwataja kama mashujaa na watafiti yalihobea katika nyanja ya utafiti na afya.
Rais wa Shirika la Ukimwi Duniani, Francoise Barre-Sinoussi alisema hata baada ya mkasa huo washiriki wataendelea kufanya vikao wakiwa na lengo la kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi.
Shirika la Afya Duniani(WHO) pia limepata pigo baada ya msemaji wake Glenn Thomas ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mwadishi wa Shirika la Utangazaji la BBC .
Glenn raia wa uingereza alipenda sana kuangazia maswala ya afya na alitumika katika shirika la WHO kwa miaka kuni.Kwa hakika viti vyao vilibaki wazi huku vitambulisho vyao vikibaki mezani huku majukumu waliotengewa katika mkutano huo yakatekulezwa na wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni