Mkutano unatarajiwa kuanza jumapili mjini Melbourne, Australia.watalaamu wa afya na watafiti wa makali ya ukimwi duniani kote wamealikwa.
Habari njema ni kuwa maambukizi ya ukimwi imepunguka kote ulimwenguni .
Shirika la Ukimwi duniani linabaini kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na ukimwi duniani vimepungua kwa kasi mwaka 2013 sawa na asilimia 11.8% ndani ya mwaka mmoja.
Zaidi ya hayo UNAIDS inasema kwamba lengo la pambano hilo mwaka huu ni kusisitiza kuwahudumia waliosahauliwa kama vile wafungwa, wafanyabiashara ya ngono, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kadhalika.
Hii ni idadi ya waathiriwa wa ukimwi duniani ambayo imetolewa na taasisi ya Umoja wa Mataifa inayokabiliana na ukimwi katika ripoti ya mwaka 2013, kabla ya kikao cha Melbourne kuhusu ukimwi.
Kwa
jumla mwaka 2013, takribani watu milioni 35 walikua wakiishi na virus
vya ukimwi duniani, huku watu milioni 1.5 walifariki kutokana na ukimwi
mwaka 2013.Mwaka huo huo wa 2013, watu milioni 2.1 duniani waliambukizwa
virus vya ukimwi, huku idadi hio ikishuka mwaka 2001 kwa asilimia
38.Watoto 240.000 walizaliwa na virus vya ukimwi mwaka 2013, huku
asilimia 87.7 wakiwa ni watoto kutoka katika nchi za Afrika ziliyoko
kusini mwa jangwa la Sahara.
Ugonjwa wa kifua kikuu ni moja ya sababu kuu ya vifo kwa watu wanaoathika na virus vya ukimwi.Dola bilioni 19.1 ziliwekezwa mwaka 2013 kwa kupambana na ugonjwa wa ukimwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni