- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Machapisho
Saratani ya tumbo
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Aliyekuwa mtangazaji mashuhuli wa kituo change habari cha Royal Media Waweru Mburu ameaga dunia. Waweru amefariki baadaya ya kuugua saratani ya tumbo. Alitumika kwenye Radio Citizen kwa miaka zaidi ya kumi na tano, huku akiwa na umaarufu kufuatia kipindi chake cha yaliyotendeka. Kabla yakufa kwake hiyo jana jioni, Waweru alitangaza nia yake ya kuwania kiti cha kisiasa katika eneo la maragua, jimbo la Murang'a. saratani ya tumbo ni saratani inayotokea katika mfuko was chakula unaosiaga na kutunza chakula kwa muda. Saratani hii hutokea katika tezi za gastric gland. Kulingana na takwimu za afya,saratani hii inatokea sana katika nchi za Japani na China Kinachosababisha saratani ya tumbo ? Wataalamu wa afya hawana uhakika nini husababisha saratani hii.Hata hivyo, Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya chakula kuchomwa, chenye chumvi nyingi au kilichohifadhiwa kwenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo.. saratani ya tumbo imepungua sana ha...
breastfeeding week
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
maziwa ya mama ndicho chanzo bora zaidi cha lishe kwa watoto wachanga,hata hivyo kuna badhi ya akina mama ambao hawapendi kamwe kuwanyonyesha watoto wao kwa sababu za kutaka kuhifadhi umbo la titi. Lakini mashirika ya kiafya yanaendelea kuwahimiza akina mama kuwanyonyesha watoto ili kuepuka maradhi na kumpa moto afya bora . Pia ni muhimu kwa akina mama ili kuepuka maradhi kama vile saratani ya titi au maradhi mengine kama vile msongo wa mawazo ambao hupata akina mama wengi baada ya kujifungia. Kulinga na utafiti wa WHO ambayo imetolewa kwa ajili ya wiki ya kunyonyesha duniani , ni nchi chache tu ambazo hutekeleza mfumo wa kimataifa, unaolenga kuzuia matangazo ya lishe mbadala kwa watoto. Akina mama ambao hufanya kazi hasa katika mashirika tofauti huwa na ungumu wa kupata muda wa kunyonyesha ,jambo ambalo huwachochea akina mama kununua na kuwapa watoto wao vyakula vya mikebe. Isitoshe,maziwa ya mama ni muhimu zaidi kumj...
Tohara Kenya
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Huku baadhi ya kabila nchini Kenya zikiendelea kupasha tohara wasichana,shirika la umoja wa mataifa limetaja kitendo hikikama dhuruma kwa watoto. Daktari Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa UNPF ametaja ukeketaji kama kitendo cha unyama na dhuruma kwa mtoto. Alisema kuna haja ya wadau kutafuta mikakati itakayo hakikisha unyama huu imekomeshwa katika sehemu au mataifa yanaoendelea kutekeleza uovu huu,hasabara la afrika abako takwimu zinaonyesha hali ni mbaya. Mataifa ya jamhuri za kiislamu,Afrika Mashariki,Magharibi na Kusini ni baadhi ya maeneo ambayo yangali yanakubatia mila na tamaduni potovu za ukeketaji. Alisema shirika lake linatafuta mikakati na sheria ya kuhakikisha swala hili limekomeshwa kabisa. Hii ni baada ya muda wa miaka ishirini ambapo mashirika ya kiserikali nay ale ya haki za kibinadamu yakikasifu tabia ya ukeketaji barani Afrika .
TB kenya
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kiwango kikubwa cha watu wanaogua ugonjwa wa kifua kikuu wamekuwa wakipatikana na Virusi Vya Ukimwi.Aidha kuchangia vifo miongoni mwa waadhiriwa. Juhudi za kupambana na TB na maambukizi ya Ukimwi zinaendelea barani Afrika hususan nchini Kenya. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kifua kikuu kama moja wapo wa magonjwa ambukizi yanayosababisha maafa nchini. Kesi za kifua kikuu zimeongezeka Zaidi ya mara tatu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mwaka wa 2015 Zaidi ya watu elfu kumi walifariki kutokana na makali ya TB. Jimbo la Pwani ya Kenya linaongoza kwa idadi ya maambukizi ya kufua kikuu huku Nairobi,Isiolo,Kisumu na Embu zikifuata. Vile vile,Majimbo ya Samburu,Tharaka,Turkana na Kirinyaga zina idadi ya azili mia 32 ya maambukizi. Kenya imekuwa mtari wa mbele kuuthibiti ugonjwa wa Tb lakini changamoto zikiwemo wagonjwa kukataa ktafuta matibabu au kukata kumeza dawa. ilibidi serikali kuweka mikakati madhubuti...
AIDS CONFERENCE DURBAN 2016
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kongamano la tano la kimataifa kuhusu ukimwi kuanza Afrika Kusini Kongamano kuhusu ukimwi liaanza mjini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wajumbe na wataalam kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Mkutano huo unafanyika wakati ambapo selikali ya Kenya imejitahidi kukabiliana na makali yake. Siku chake zilizopita, wizara ya afya Kenya, ilianzisha sera na kampeini ambayo itawasaidia wanaougua na wanaofahamu hali yao ya HIV kupata tiba mara moja.Kampeini inayo ; anza sasa pia itawezesha watoto wanaozaliwa na virusi vya HIV kuanza matibabu mara moja. Lakutia moyo ni kwamba idadi ya maabukizi nchini Kenya imepungua,huku Afrika kusini hasa Durban ambapo mkutano huu unafanyika hali ikiwa sio nzuri. Zaidi ya hayo,Utafiti unaonyesha watu milioni 40 ulimwenguni walioambukizwa virusi vya ukimwi wanatokea barani Afrika. Serikali ya kenya imetenga shilingi bilioni 22 kupambana na janga h...