Machapisho

Tohara Kenya

Huku baadhi ya kabila nchini Kenya zikiendelea kupasha tohara wasichana,shirika la umoja wa mataifa limetaja kitendo hikikama dhuruma kwa watoto. Daktari Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa UNPF ametaja ukeketaji kama kitendo cha unyama na dhuruma kwa mtoto. Alisema kuna haja ya wadau kutafuta mikakati itakayo hakikisha unyama huu imekomeshwa katika sehemu au mataifa yanaoendelea kutekeleza uovu huu,hasabara la afrika abako takwimu zinaonyesha hali ni mbaya. Mataifa ya jamhuri za kiislamu,Afrika Mashariki,Magharibi na Kusini ni baadhi ya maeneo ambayo yangali yanakubatia mila na tamaduni potovu za ukeketaji. Alisema shirika lake linatafuta mikakati na sheria ya kuhakikisha swala hili limekomeshwa kabisa. Hii ni baada ya muda wa miaka ishirini ambapo mashirika ya kiserikali nay ale ya haki za kibinadamu yakikasifu tabia ya ukeketaji barani Afrika .

TB kenya

Kiwango kikubwa cha  watu wanaogua ugonjwa wa kifua kikuu wamekuwa  wakipatikana  na Virusi Vya Ukimwi.Aidha kuchangia vifo miongoni mwa waadhiriwa. Juhudi za kupambana na TB na maambukizi ya Ukimwi zinaendelea  barani Afrika hususan nchini Kenya. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kifua kikuu kama moja wapo wa magonjwa ambukizi yanayosababisha maafa nchini. Kesi za kifua kikuu zimeongezeka Zaidi ya mara tatu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mwaka wa 2015 Zaidi ya watu elfu kumi walifariki kutokana na makali ya TB. Jimbo la Pwani ya Kenya linaongoza kwa idadi ya maambukizi ya kufua kikuu huku Nairobi,Isiolo,Kisumu na Embu zikifuata. Vile vile,Majimbo ya Samburu,Tharaka,Turkana na Kirinyaga zina idadi ya azili mia 32 ya maambukizi. Kenya imekuwa mtari wa mbele kuuthibiti ugonjwa wa Tb lakini changamoto zikiwemo wagonjwa kukataa ktafuta matibabu au kukata kumeza dawa. ilibidi serikali kuweka mikakati madhubuti...

AIDS CONFERENCE DURBAN 2016

Picha
Kongamano la tano la kimataifa kuhusu ukimwi kuanza Afrika Kusini Kongamano kuhusu ukimwi liaanza   mjini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wajumbe na wataalam kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Mkutano huo unafanyika wakati ambapo   selikali ya Kenya imejitahidi kukabiliana na makali yake.   Siku chake zilizopita, wizara ya afya Kenya, ilianzisha sera na kampeini ambayo itawasaidia wanaougua na   wanaofahamu hali yao ya HIV kupata tiba mara moja.Kampeini inayo ; anza sasa pia itawezesha watoto wanaozaliwa na virusi vya HIV kuanza matibabu mara moja.   Lakutia moyo ni kwamba   idadi ya maabukizi nchini Kenya imepungua,huku Afrika kusini hasa Durban ambapo mkutano huu unafanyika hali ikiwa sio nzuri.   Zaidi ya hayo,Utafiti unaonyesha   watu milioni 40 ulimwenguni walioambukizwa virusi vya ukimwi wanatokea barani Afrika.   Serikali ya kenya imetenga shilingi bilioni 22 kupambana na janga h...

homa ya mapafu(Pneumonia)

Picha
Pneumonia Homa ya mapavu ni ugonjwa ambao unaathiri mapafu na unaua watoto kwa wingi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Ugonjwa wa nimonia umetajwa kuwa ugonjwa hatari na unauwa kwa kasi sana,huku idadi ya maafa yakiongezeka kila siku. nchini Kenya. Ripoti ya wizara ya afya ,Kenya inasema kuwa idadi ya wanaofariki imeongezeka maradufu. Pia watoto wameathirika Zaidi,inakadiriwa kwamba watu karibu 21,640 walifariki mwaka wa  2013 huku idadi ikiongezeka hadi  22,473 mwaka uliopita wa 2015. Hii ni changamoto kwa sekta ya afya kwani kuna mbinu za kupunguza makali ya nimonia.  vifo hivi vinavyotokana na homa ya mapafu(nimonia) ,vinaripotiwa wakati madaktari na wauguzi wamekuwa wakifanya migomo kulalamikia mishahara duni na pia mazingira mabaya ya kufanyia kazi. Hii ni jambo ambalo si la kuchangamkiwa ,na ni sharti wizara ya afya itekeleze majikumu yake ipasavyo. Ni husuni kusuhudia maafa ya kila mara ,hasa kwa waz...

Malaria Kenya

Picha
Idadi ya wagonjwa wa   malaria yapungua Kenya Ugonjwa wa malaria umekuwa ni tisho katika maeneo yenye joto Afrika hususan nchini Kenya. Jambo la kutia moyo ni kwamba   iadadi ya watu wanaougua ugonjwa huu umepungua marudufu kwa miaka sita iliyopita. Kulingana na tafiti za wizara ya Afya hali hii inatokana na ongezeko la utumiaji viandarua na pia kupata matibabu mapema.Msemaji wa wizara ya afya Elisha Omondi anasema hatua za serikali za kuukabili ugonjwa wa malaria zimezaa matunda. Hata hivyo sehemu kama vile   jimbo la Siaya linaongoza kwa maambukizi hayo,lakini pia katika kipindi cha mwaka mmoja angalau asilimia 50 ya visa vimekabiliwa. Majimbo ya Pwani pia yameadhirika lakini hali sio mbaya kama siku za nyuma. Takwimu sinaonyesha kuwa Malaria iliwaua karibu watu nusu milioni duniani mwaka jana, huku vifo tisa juu ya kumi vikitoka kusini mwa Sahara. Kenya ni miongoni mwa mataifa ya kusini mwa Jangwa la Afrika ambapo Malaria imeandelea kuangamiza watu lak...

Mama Lucy KIbaki

Picha
Aliyekuwa mama wa taifa Aaga dunia Baada ya kifo chake aliyekuwa Mama wa taifa nchini Kenya,watu wa tabaka mbali mbali wameendelea kutakia familia yake afueni,huku wakimumiminia sifa kama mama wenye bidiina aliyewajali wasiojiweza. Juhudi zake za kuunda muungano wa akina mama wa marais afrika ili kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ni mfano wa mama aliyewajali wengine. Pia alikuwa mstari wa mbele kuhakikisa maswala na afya ya uzazi imeimarishwa.Aliwatembelea wagonjwa hospitalini na aliyoyaona hasa mazingira mbaya wagonjwa waliokuwemo yalimtamausha. Alinena kwa hasira na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa maafisa wa selikali wafisadi . Hospitali ya mama Lucy ilijengwa kwa heshima zake na wakaazi wa Embakazi wana sababu kushukuru kwa hayo."ukakamavu wake mama na bidii katika maswala la afya ilifanya sisi tupate hospitali karibu,tunafurahi sana,alisema Monica Wahito . John Kariuki anasema ,''hospitali ya mama Lucy imekuwa na sifa mbaya ya kutekelezwa kwa waogojwa ...