Jumatano, 28 Septemba 2011

Ovarian Cancer(saratani ya mfuko wa mayai)


Hii leo nitaandika zaidi na kuwaelimisha kuhusu saratani ya mfuko wa mayai yaani ovarian cancer.

Je wajua kuhusu Saratani ya kifuko cha mayai ya uzazi ?
Mwanamke ana vifuko viwili vidogo vilivyo kila upande wa  mfuko wake wa uzazi.Kwa mujibu wa tafiti,ni vigumu kuitambua saratani hii.

Hivyo basi ni muhimu kutembelea daktari kila mwaka kwa uchukuzi wa kina.Dalili zake huonekana ugonjwa ukiwa umeenea mno.

Walio  kwenye hatari ya kupata saratani hii ni

v     -Wanawake wenye zaidi ya umri wa miaka 50 wako hatarini ya kuambikizwa ugonjwa huu.

v     mwanamke tasa
v     Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya matiti
v     Ikiwa kuna mtu wa familia ambaye amewahi kuugua ugonjwa huu.
v     Kupata hedhi katika umri mdogo

Hata hivyo, kama saratani yingine,inapogunduliwa mapema mtu anaweza kupona.

Ni muhimu kula vyakula kama mboga, matunda ambavyo vinafahamika kupunguza hatari ya saratani.

Ni vigumu kupata takwimu kamili za akina mama wanaougua ugonjwa huu au maafa kwani Wanawake wengi hasa wa mashinani, wanafariki bila kufahamu wanaugua saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi.

Pia gharama ya kujitibisha ni ya juu mno.Hivyo basi ni wachache wana uwezo wakugharamia matibabu ya Saratani.

Zaidi ya hayo, kuna haja ya kuelimisha akina mama umuhimu wa kutafuta matibatu au kuchunguzwa katika sehemu ya uzazi mara kwa mara.

Wizara ya Afya pia ina jukumu ya kufanya kampeini ili kuukabili au kuangamiza ugonjwa wa saratani nchini.

wasifu wa Mama Wangari Maathai


Taarifa ya  kifo cha aliyekuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Wangari Maathai, imepokelewa kwa huzuni.
Watu wa tabaka mbalimbali wamenukuliwa wakitoa rambi rambi zao, huku wakimumiminia sifa chungu nzima .
Ni wazi kuwa  kifo chake Maathai si pigo tu kwa wanaharaki wa mazingira nchini Kenya lakini kwa ulimwengu wote.




Prof.Maathai akipanda mti
Mama Mathaai aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi  alikokuwa akitibiwa saratani ya mfuko wa uzazi(Ovarian Cancer)

Umaarufu wa Mathaai ulitokana na ari yake ya Mazingira.Alikuwa kwenye mstari wa mbele kuelimisha wakenya na ulimwengu kwa ujumla umuhimu wa  kuhifadhi na kutunza mazingira.

Pia alipigia debe jitihada za kutimiza lengo la milenia la kutunza na kulinda mazingira.

Karne tatu zilizopita, Maathai aliasisi shirika la mazingira nchini Kenya, Kenya Green Belt Movement.

Alikuwa mama shujaa na pia  mkakamavu ambaye hakutishwa na yeyote.Alifanya kazi yake aliyoienzi kwa dhati.

Wanyakuzi alihakikisha mipango yao imetibuliwa.Alifanya kampeni ya kupinga ujenzi wa majengo mawili katika bustani ya Uhuru.

Zaidi ya hayo, aliandamana na wanaharakati wa mazingira hadi Mlima Kenya kungoa bangi.Shughuli ya upandaji bangi ndani ya msitu wa mlima Kenya ilikuwa imekidhiri hadi alipoingilia kati.

Maathai alikuwa mashuhuri kote duniani na alipanda miti popote alipozuru.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004 na kuwa mwanamke wa kwanza mwafrika, mkenya wa kwanza na mwanamazingira wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo.

chemichemi ya maji

 Mwaka wa 2002, aliibuka mshindi wa kiti cha ubunge cha Tetu.Vilevile,aliteuliwa na rais Mwai Kibaki kuwa naibu waziri  wa mazingira, wadhifa alioushikilia hadi mwaka mwa 2005.

Baadhi ya Viongozi mashuhuli waliotuma rambirambi zao ni;

Rais wa Marekani, Barak Obama
Nelson Mandera,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nataifa
Kofi Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Achin Steiner,Mkurugenzi kuu wa Shirika la Mazingira Ulimwenguni.









Prof.Wangari Mathaai


Kifo cha shujaa wa Mazingira


Mama Wangari Maathai
Hongera Mama Mathaai kwa kazi yako nzuri ulioifanya.
Chemichemi za maji ukahakikisha zimelindwa.
Shughuli ya ukataji miti misituni ukapigwa marufuku.
Upanzi wa bangi Mlima Kenya ukakoma.


Majereha ukapata kwa ajili ya mangizira.
Katunukiwa Tuzo ya Nobeli kwa ukakamavu wako
Hongera! Hongera! Mama Mathaai
Mola akuweke pema peponi.

Jumatatu, 26 Septemba 2011

Polio(ugonjwa wa kupooza)



Serikali ya Kenya imezindua kampeini ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa upooza Septemba 23, 2011.Kampeni hiyo inalenga maeneo ambaye dalili ya ugonjwa huu imeanza onekana,kama vile Migori, Homa-Bay, Kisii, Nyamira na Transmara. .watoto walio chini ya miaka mitano watachanjwa.

Hivi majuzi waziri wa Afya ya Umma, Beth Mugo alitangaza kuwa Kenya inakabiliwa na hatari  ya mkurupuko wa ugonjwa wa kupooza baada ya kijana mwenye umri wa miaka mitatu kupatikana virusi ya polio katika Wilaya ya Rongo, Mkoani Nyanza.

Ugonjwa wa polio husababiswa na virusi na kwa hivyo ni vingumu kutibiwa, punde tu mtu anapoambukizwa.

Mwongozo wa shirika la Afya duniani(WHO) unabainisha kuwa ili kudhibiti mzunguko wa virusi pori vya ugonjwa wa kupooza,ni muhimu kutoa chanjo za zaidi kwa njia ya kampeni kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 angalau kwa awamu mbili.

Chanjo hii inatolewa na wataalam wa afya kwa njia ya matone kinywani kwa watoto wote, bila kujali kama walipata chanjo hiyo hapo awali au hawakupata.

Adhari za ugonjwa wa kupooza(polio)

Akiwa na umri wa miaka ishirini na tano John Katana anaugua ugonjwa wa kupooza.Katana ni mmoja kati ya wakenya wengi ambayo,endapo wazazi wao wangeliwapeleka kuchanjwa, hii leo wangekuwa  na uwezo wa kutembea bila matatizo yeyote.

Yeye hutumia kiti cha kukokotwa kwani  miguu yake miwili imepooza.
Alipozaliwa mamake hakutilia maanani umuhimu wa chanjo hii.Hivyo basi,hakumpeleka kupata viwango vyote vinne vya chanjo ya kupooza.

Aliwaza kuwa,mwanawe  na pia watoto wa jirani yake wamerogwa. Kijiji pale pia maradhi haya yalienea kwa kasi.huku Watoto zaidi ya kumi wakiabukizwa.

Dalili za polio
Mamake katana anasema mwanawe alianza kuumwa na kichwa, maumivu na udhaifu wa misuli. 
Kwa bahati nzuri,kampeni dhini ya ugonjwa wa kupooza ilitangazwa na serikali. Baadya ya mafuzo ya kiafya,Akagundua kumbe mwanawe alikuwa tu anaugua polio kwa sababu ya uzembe kwake.

Laiti  angalijua, Katana hangelemaa;angekuwa na afya nzuri kama watoto waliopokea chanjo wakiwawachanga.

Kwa sasa, yeye na akina mama wenzake wamechukua jukumu la kuwaelimisha wanawake umuhimu wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza.
Jinsi polio inavyoenezwa
*Watoto ambao hawajachanjwa
*virusi vya polio huenezwa  kwa kula chakula au kunywa maji machafu yalichanganyika na virusi vya polio au kwa kinyesi cha mwadhiriwa.


Alhamisi, 22 Septemba 2011

saratani ya shingo ya uzazi (Cervical cancer)


 Ikiwa kuna ugonjwa ambao unasababisha vifo vya  wanawake wengi hapa nchi na duniani kwa ujumla, basi si mwingine ila ule wa saratani.
Kuna aina kadhaa za saratani zinazo waathiri wanawake.

Saratani ya shingo ya kizazi ni baadhi tu ya aina kadhaa za ugonjwa huu hatari.

Mama Hannah Mwendeo* anafahamu vyema jinsi ugonjwa huu umekuwa tishio kwa wanawake wengi.

"kabla madaktari kugundua maradhi niliyokuwa nikiugua, nilikuwa nina maumivu sana.Pia nilikuwa napata hedhi kila wakati,lakini si kufahamu kwamba nilikuwa tayari naugua saratani ya shingo ya uzazi.

Kwa bahati nzuri.watalamu wa afya walitambua ni saratani ya shingo ya uzazi na papo hapo alianza matibabu".

Kwa sasa amepona na anatowa wito kwa aki mama wenzake wajipimishe mapema ili kuepana na hatari au tishio la ugonjwa huu.

Takwimu zilizotolewa na  shirika la afya duniani (WHO) , asilimia 3.2 ya wanawake nchini Kenya, walio kati ya miaka 18-69 hupimwa kila baada ya miaka mitatu ikilinganishwa na wanawake asilimia 70 wanaoishi katika nchini zilizoendelea.


Kulingana na tarifaa za WHO ugonjwa huu unasabambishwa na virusi viitwavyo Human Papiloma (HPV) ambavyo dalili zake huanza kuonekana miaka kumi baada ya mgonjwa kuvipata.
 
Virusi vya Human Papilloma

Inakisiwa kuwa idadi ya wanaougua ugonjwa huu unaongezeka kasi zaidi nchini Kenya.Huku asilimia 35 wanawake wakihofiwa kuwa na virusi ya Human Papilloma.Virusi hivi huambukizwa wakati wa kujamiana au kufanya ngono ambapo mwanamke na mwanaume huambukizana virusi hivi.

Dalili za ugonjwa huu,ni pamoja na kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la ndoa, kuvuja damu hata baada ya hedhi,kuwa na maumivu wakati wa kufanya ngono na pia kutoa harufu mbaya.

Mwanamke anayekuwa na wapenzi wengi yuko hatarini yakuambukizwa au kupata maradhi haya.Pia,Kuanza ngono katika umri mdogo,uvutaji sigara na maambukizi ya magonjwa ya ngono kama vile kisonono,kasende na hata ukimwi.

Mwaka wa 2007,serikali ya Kenya ilianzisha mpango wa wanawake kujipimisha ilikutambua mapema endapo wanaugua ugonjwa huu.Pia akina mama wanashauriwa kupima kila mwaka, kwa kuwa wengi hupatwa na viashiria vya saratani hii bila wao kutambua.

Kwa kuwa kila mwanamke ambaye ameshiriki ngono yuko hatarini ya kupata na ugonjwa huu.Serikali imetoa rai kwa kila mwanamke ambaye hana ugonjwa wa saratani ya uzazi kupata chanjo inayopatikana katika vituo vya afya nchini.
Mam ahana ni baadhi tu ya wanawake waliopatikana na viashiria vya saratani ya shingo ya uzazi mapema na uwezekano wake wakupona ni asilimia 90 hadi 95 tofauti na yule .amepatikana na ugonjwa huu akichelewa. kupona ni mkubwa kwa asilimia 90 hadi 95.



Jumatano, 14 Septemba 2011

Uterine Fibroid Embolization

Uterine Fibroid Embolization

Je wajua kuwa ugonjwa wa fibroids yaani uvimbe au vivimbe  ambavyo  huwa  kwenye ukuta wa kizazi (uterus) waweza kutibiwa na mwanamke akawa hana matatizo tena kwenye uzazi wake?


Kwa mujibu wa daktari, Timona Obura, ambaye ni mtaalam (Gynaecologist) katika hospitali ya Aga Khan, Hii inawezekana kutokana na tecnhologia ya kisayansi ambayo inajulikana kama Uterine Fibroid Embolization.

Vivimbe hivyo vinaweza kuwa vidogo Kama ncha ya kidole au vikubwa Kama viasi .Pia vinaweza kugunduliwa, kwa kutumia tecnologia inayojulikana kama Ultrasound.


 
Mwanamke anaweza akawa kwenye hatari ya mimba kutoa(miscarry) kwani,uvimbe unaweza kujaa kwenye sehemu anayokaa mtoto.


Ingawa kuna  aina za upashuaji zinazotumiwa kuondoa Fibroids,Daktari Obura anasisitiza kuwa Embolization ni namna maalum ambayo haihitaji upasuaji wa kawaida.Pia hamna madhara kama upasuaji wa kawaida.

Hapa mwanamke au mgonjwa anaelimishwa kuhusu jinsi upasuaji unavyofanywa,faida na jambo lolote analostahili kufahamu kabla hajafanyiwa upasuaji.

Hii binu ni muhimu kwa wale wanaotarajia kupata watoto siku za badaye.Pia kuna afueni kwani fibroids hazirudi tena.

Hata hivyo kuna  upasuaji kama vile  (Hysterectomy) hapa mwanamke anatolewa kizazi chote na hawezi kutunga mimba tena.Hii hufanywa kwa mwanamke ambaye   Fibroid ni kubwa ,nyingi na pia hana haja au lengo la kuzaa tena.


 Myomectomy ni namna pia ya upasuaji, ambapo mwanamke hutolewa  Fibroids tu na kuacha kizazi.Ikiwa  Fibroid ni moja au chache na si kubwa sana, mwanamke anaweza kuendelea kuzaa.Hii ni shuluhu ya muda tu kwa maana fibroids zinaweza zikarudi.

Kuzuia ni bora kuliko kuponya,wale wanaugua ugonjwa huu wanaweza kuamua wenyewe au kwa usaidizi wa Gynaecologia wake.

Pia ni muhimu kutafuta matibabu ya haraka unapougua,kuepukana na hatari.

-Dalili za ugonjwa wa Fibroids ni kama vile kuvuja damu kwa wingi wakati wa hedhi na Kuumwa na tumbo.

Kwa mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa fibroid tutakuwa kunaalika maoni kutoka kwa mashabiki wanaotembelea mtandao huu.

Yote mwakaribishwa kutoa maoni au kuuliza swali.

Jumatatu, 12 Septemba 2011

Obstetric fistula

Fistula
Katika baadhi ya mikoa hapa nchini Kenya, akina mama waja wazito hulazimika kutembea  mwendo  mrefu kutafuta matibabu.Baadhi yao  hulazimika kujifungua nyumbani ,jambo ambalo husababisha madhara ya kiafya.

Uchungu wa muda mrefu,kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu  au kujifungua katika mazingira yasiyofaa ni chanzo cha ugonjwa unaojulikana kama fistula.
Kulingana na daktari wa afya ya uzazi katika hospitali moja hapa jijini Nairobi,Fistula ni tatizo linalotokana na jeraha wanalopata kina mama wakati wa kujifungua baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na pia kuwa na njia ndogo ya uzazi kiasi kwamba kichwa cha mtoto kinashindwa kupita kwa usalama wakati wa kujifungua.

Hali hii humfanya mama kushindwa kujizuia wakati anapotaka kwenda haja ndogo na wakati mwingine hata kubwa bila mpangilio.

Ugonjwa huu ,umehatarisha maisha ya akina mama wengi.

 
Wengi wao hutengwa na jamii kwani wanakuwa hawawezi kufanya lolote,na pia wanatoa harufu inayosambabishwa na kuvuja kwa mkojo.Hawana uwezo wakuzuia haja kubwa wala ndogo.

Takwimu za Shirika Afya Duniani (WHO) sinadhihirisha ya kuwa zaidi ya  wanawake milioni nne ulimwenguni kote wanaishi na fistula .
Daktari wanatilia mkazo  haja ya wanawake wajawazito  kutembelea kliniki za afya mara tu wanapotunga mimba ,ili kupata utalamu na mawaidha ya afya,hili kupunguza hatari.
Nchini Kenya kuna baadhi ya mashirika ya afya yaani mashirika yashiyo ya serikali ,yanayotoa matibabu ya bure kwa baadhi wa wanawake ambao wamejikuta kwenye lindi hili na masonokeko.

Jambo la kutia moyo ni kuwa tatizo hili linaweza kutatuliwa.Baadhi ya wanawake niliowahoji wanasema kuwa baada ya  upasuwaji na watalaamu wa afya ya uzazi,walirejea katika hali zao za kawaida.

afya ya uzazi

 

Kuna haja ya kutoa elimu ya afya ya uzazi shuleni.Ili kupunguza ongezeko la Ujauzito
Kwa vijana wakiwa wadogo.

Kulingana na mila na tamaduni za kiafrika baadhi wa walimu na pia wazazi hawataki kuzungumzia maswala ya ngono kwa watoto.

Hizi ni mila ambazo zimepitwa na wakati na ni jukumu   letu kulitilia maanani  elimu ya afya ya uzazi.

Kulingana na watalamu ya afya, unaweza kutungwa mwanamke au msichana mimba  anapokaribia kupata hedhi kufanya tendo la ndoa pasipo kutumia mbinu yoyote ya kuuzuia.
Hivi majuzi visa vya wasichana wa chini ya miaka kumi kutunga mimba  vimeripotiwa nchini Kenya.
La kusikitisha ni kwamba wengi hawana habari kuhusu afya ya uzazi
Pia waohupata  matatizo ya kujifungua kwani viungo vyao kama vile mishipa ya uzazi haijakomaa.
Zaidi ya hayo,ugonjwa wa fistula unaweza ukatokea baada ya kujifungua.
Kwa hivyo elimu ya afya ya uzazi ni muhimu zaidi kwa kundi hili la vijana wasichana kwa wavulana.
Hivyo basi, kuna haja ya  walimu shuleni, pamoja na wataalamu wa afya kutoka serikalini na mashirika binafsi kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana na wavulana ili waweze kuepuka matatizo yayoweza kuwakumba wakiwa wadogo.

Kulingana na elimu ya kisayanisi, wavulana wanapobalehe wanaweza kutoa mbegu za uzazi zenye uwezo wa kutunga ujauzito.
Hii ni wazi kuwa  wavulana, hata wakiwa kwenye miaka kumi na kuendelea, wanaweza kumtunga msichana au mwanamke ujauzito!

Jinsi ya kujiepusha  kupata mimba?

Kuijikinga kwa kutumia mbinu au mikakati tofauti ya upangaji  uzazi
Kutojihuzisha na tendo la ngono kabla ya kuingia katika ndoa.


afya ni uhai

Afya ni uhai

Mazingira machafu ni chimbuko la magonjwa chungu nzima.
Mamia ya watu kote duniani, huadhirika kiafya na hata kufariki kufuatia hali hii.

Hivyo basi, ni jukumu la kila mtu kuhakikisha ya kwamba hali ya usafi unadumishwa kila wakati.
Kwa mfano ugonjwa wa kipindupindu unahatarisha maisha ya watu wengi.

Waswahili husema kuwa kuzuia ni bora kuliko kuponya.Fauka ya hayo, itakuwa ni jukumu ya kila mtu kuhakikisha anaishi katika mazingira safi,ilikuepuka magonjwa kama hayo.



Kipindupindu


Kipindupindu ni kuharisha papo hapo.Huu ni ugonjwa  ambao unaweza kuua ndani ya masaa kama ukiachwa bila kutibiwa.


Mara tu baada ya  ugonjwa kupatikana  ni jambo la  muhimu kutafuta matibabu ya haraka.

Utoaji au utumiaji wa maji safi,vyoo bora na elimu ya afya kwa umma na usafi wa mazingira,ni baadhi tuu ya  namna ya kupunguza madhara au kukabiliana na tishio la ugonjwa wa kipindupindu.


Afya yako iko mikononi mwako.Kampeni ya kuosha mikono baada ya kwenda chuooni ni muhimu.