Ikiwa kuna ugonjwa ambao unasababisha vifo vya wanawake wengi hapa nchi na duniani kwa ujumla, basi si mwingine ila ule wa saratani.
Kuna aina kadhaa za saratani zinazo waathiri wanawake.
Saratani ya shingo ya kizazi ni baadhi tu ya aina kadhaa za ugonjwa huu hatari.
Mama Hannah Mwendeo* anafahamu vyema jinsi ugonjwa huu umekuwa tishio kwa wanawake wengi.
"kabla madaktari kugundua maradhi niliyokuwa nikiugua, nilikuwa nina maumivu sana.Pia nilikuwa napata hedhi kila wakati,lakini si kufahamu kwamba nilikuwa tayari naugua saratani ya shingo ya uzazi.
Kwa bahati nzuri.watalamu wa afya walitambua ni saratani ya shingo ya uzazi na papo hapo alianza matibabu".
Kwa sasa amepona na anatowa wito kwa aki mama wenzake wajipimishe mapema ili kuepana na hatari au tishio la ugonjwa huu.
Takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani (WHO) , asilimia 3.2 ya wanawake nchini Kenya, walio kati ya miaka 18-69 hupimwa kila baada ya miaka mitatu ikilinganishwa na wanawake asilimia 70 wanaoishi katika nchini zilizoendelea.
Kulingana na tarifaa za WHO ugonjwa huu unasabambishwa na virusi viitwavyo Human Papiloma (HPV) ambavyo dalili zake huanza kuonekana miaka kumi baada ya mgonjwa kuvipata.
Virusi vya Human Papilloma |
Inakisiwa kuwa idadi ya wanaougua ugonjwa huu unaongezeka kasi zaidi nchini Kenya.Huku asilimia 35 wanawake wakihofiwa kuwa na virusi ya Human Papilloma.Virusi hivi huambukizwa wakati wa kujamiana au kufanya ngono ambapo mwanamke na mwanaume huambukizana virusi hivi.
Dalili za ugonjwa huu,ni pamoja na kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la ndoa, kuvuja damu hata baada ya hedhi,kuwa na maumivu wakati wa kufanya ngono na pia kutoa harufu mbaya.
Mwanamke anayekuwa na wapenzi wengi yuko hatarini yakuambukizwa au kupata maradhi haya.Pia,Kuanza ngono katika umri mdogo,uvutaji sigara na maambukizi ya magonjwa ya ngono kama vile kisonono,kasende na hata ukimwi.
Mwaka wa 2007,serikali ya Kenya ilianzisha mpango wa wanawake kujipimisha ilikutambua mapema endapo wanaugua ugonjwa huu.Pia akina mama wanashauriwa kupima kila mwaka, kwa kuwa wengi hupatwa na viashiria vya saratani hii bila wao kutambua.
Kwa kuwa kila mwanamke ambaye ameshiriki ngono yuko hatarini ya kupata na ugonjwa huu.Serikali imetoa rai kwa kila mwanamke ambaye hana ugonjwa wa saratani ya uzazi kupata chanjo inayopatikana katika vituo vya afya nchini.
Mam ahana ni baadhi tu ya wanawake waliopatikana na viashiria vya saratani ya shingo ya uzazi mapema na uwezekano wake wakupona ni asilimia 90 hadi 95 tofauti na yule .amepatikana na ugonjwa huu akichelewa. kupona ni mkubwa kwa asilimia 90 hadi 95.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni