Jumatano, 28 Septemba 2011

wasifu wa Mama Wangari Maathai


Taarifa ya  kifo cha aliyekuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Wangari Maathai, imepokelewa kwa huzuni.
Watu wa tabaka mbalimbali wamenukuliwa wakitoa rambi rambi zao, huku wakimumiminia sifa chungu nzima .
Ni wazi kuwa  kifo chake Maathai si pigo tu kwa wanaharaki wa mazingira nchini Kenya lakini kwa ulimwengu wote.




Prof.Maathai akipanda mti
Mama Mathaai aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi  alikokuwa akitibiwa saratani ya mfuko wa uzazi(Ovarian Cancer)

Umaarufu wa Mathaai ulitokana na ari yake ya Mazingira.Alikuwa kwenye mstari wa mbele kuelimisha wakenya na ulimwengu kwa ujumla umuhimu wa  kuhifadhi na kutunza mazingira.

Pia alipigia debe jitihada za kutimiza lengo la milenia la kutunza na kulinda mazingira.

Karne tatu zilizopita, Maathai aliasisi shirika la mazingira nchini Kenya, Kenya Green Belt Movement.

Alikuwa mama shujaa na pia  mkakamavu ambaye hakutishwa na yeyote.Alifanya kazi yake aliyoienzi kwa dhati.

Wanyakuzi alihakikisha mipango yao imetibuliwa.Alifanya kampeni ya kupinga ujenzi wa majengo mawili katika bustani ya Uhuru.

Zaidi ya hayo, aliandamana na wanaharakati wa mazingira hadi Mlima Kenya kungoa bangi.Shughuli ya upandaji bangi ndani ya msitu wa mlima Kenya ilikuwa imekidhiri hadi alipoingilia kati.

Maathai alikuwa mashuhuri kote duniani na alipanda miti popote alipozuru.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004 na kuwa mwanamke wa kwanza mwafrika, mkenya wa kwanza na mwanamazingira wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo.

chemichemi ya maji

 Mwaka wa 2002, aliibuka mshindi wa kiti cha ubunge cha Tetu.Vilevile,aliteuliwa na rais Mwai Kibaki kuwa naibu waziri  wa mazingira, wadhifa alioushikilia hadi mwaka mwa 2005.

Baadhi ya Viongozi mashuhuli waliotuma rambirambi zao ni;

Rais wa Marekani, Barak Obama
Nelson Mandera,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nataifa
Kofi Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Achin Steiner,Mkurugenzi kuu wa Shirika la Mazingira Ulimwenguni.









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni